Nina mashaka na uraia wa ndugu Wallace Karia

Nina mashaka na uraia wa ndugu Wallace Karia

Rozela

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2024
Posts
845
Reaction score
2,235
Vyombo vya ulinzi na usalama especially Uhamiaji, lichunguzeni hili.
===
MAJIBU YA IDARA YA UHAMIAJI KUHUSU URAIA WA WALLACE KARIA

Mnamo Agosti 03, 2017 Msemaji wa uhamiaji Ally Mtandu alitoa uthibitisho wa uraia wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la soka TFF Wallace Karia kuwa ni mtanzania kutoka upande wa mzazi wake mmoja na tangu alipokua alichagua uraia wa Tanzania. Taarifa hizo zilitolewa na ofisi hiyo ya uhamiaji baada ya Mmoja wa wagomea wa kiti hicho kutoa taarifa kwamba Karia si Mtanzania huku akikosa vithibitisho kuonyesha kama si Mtanzania.

Kwa msingi huo Bwana Karia Alikuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha (51) na (2) cha sheria ya Uraia ya Tanzania sura ya 357 (Rejeo la 2002) na kanuni zake wakati huohuo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi.

View attachment 3262234
 
Wallaca karia ni Mtanzania mzaliwa wa tanga, lakini Mama yake ni mtu wa morogoro hukooo mchamba matope mvomero, aliyeanza kujishughulisha na soka akiwa na miaka 20 tu, na kuingia kama katibu pale tff 2017 ndio kuchaguliwa uraisi tff.
An ndugu zake wengi sana pale Morogoro wenye nyadhifa mbali mbali za juu.
Hawa walikua watu wakujiongeza miaka hiyo ya 200-2004.
Hivo usije ukatia shaka kabisa kuhusu karia. Kalowea kweli kweli kwenye jimbo la abood.
Hawa walikuja mjini na scandinavia.
 
Umeanza kuwa na Mashaka nae baada ya yeye kuanza kuwafungia watu Kama Manara, Ally Kamwe , Jerry Muro n.k

Kazi ya Mpira hasa kuwa spoken men (Msemaji) sifikirii Kama ni ngumu kiasi cha kumfanya mtu kuingia katika 18 za TFF Ila naamini yatapita pia Kijana Kama Ally Kamwe awe makini hiyo nafasi yake wanahitaka watu wengi.
 
Mnamo Agosti 03, 2017 Msemaji wa uhamiaji Ally Mtandu alitoa uthibitisho wa uraia wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la soka TFF Wallace Karia kuwa ni mtanzania kutoka upande wa mzazi wake mmoja na tangu alipokua alichagua uraia wa Tanzania. Taarifa hizo zilitolewa na ofisi hiyo ya uhamiaji baada ya Mmoja wa wagomea wa kiti hicho kutoa taarifa kwamba Karia si Mtanzania huku akikosa vithibitisho kuonyesha kama si Mtanzania.

Kwa msingi huo Bwana Karia Alikuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha (51) na (2) cha sheria ya Uraia ya Tanzania sura ya 357 (Rejeo la 2002) na kanuni zake wakati huohuo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi.

Mi na wasiwasi na kizimkazi na waarabu sio kwa wingi huu kuja wengi
 
Kwa kumuangalia tu usoni huwezi kuuliza kama ni Msomali, au la! The same to Hussein Bashe.
 
Huu ni ubaguzi wa kingese wa watu walio na mawazo finyu,na wavivu wa kufikiri...Iwe ni raia au sio raia Mwafrica anaweza kuwa popote katika Afrika.

Ni hawa wenye kujisifu kuhusu Marekani kuwa na democrasia kiasi cha kuruhusu Watu Kama kina Obama,na Kamalla kudhika nyadhifa za juu katika Nchi.

Hawa hawa wanasuport Serkali Pumbavu ya Kinshasa Kusema Banyamulenge sio Raia wa Kongo!Mwafrica ni nani katika Africa????

Mwalim,hakuwa mjinga kumjumuisha Joseph Mungai Serkalini...wala umuajiri Mghana...Hii ilidhiirisha Pan Africanism......

Tanzania tumeshinda vita vya Ukabila...ni kwa nini tuhoji Uraia wa Mwafrika????

Amandla!!!
 
Hata kama asili yake sio mtanzania lkn amefuata vigezo vyote vya kuwa mtanzania basi huyo ni raia halali kabisa wa nchi hii. Jamaa yuko makini sana na kimsingi ktk uongozi wake amefanya mapinduzi makubwa sana kwenye mpira wetu.
Karia ni akili kubwa sema ndo basi tu nchi yetu haina mifumo mizuri ya kuwatumia watu wenye uwezo mkubwa kutumia uwezo wao zaidi ya mipaka ya watawala. Lzm uwe chawa kwanza ama uwasifie sifie ndo utafanya kazi ktk mazingira mepesi kidogo
 
Mda wake wa kuhudumu unaenda kuisha ebu muache mzee wa watu aje kula pensheni yake vzr.

Wacha mzee akule pesa zake za ustaafu kwa amani sasa unataka propaganda ili iweje kua na shukran bana
 
Back
Top Bottom