#COVID19 Nina maswali haya kuhusu Chanjo za Covid-19

#COVID19 Nina maswali haya kuhusu Chanjo za Covid-19

Airmanula

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
3,527
Reaction score
5,762
Ni kwanini sisi watanzania tutumie chanjo Ya Johnson & Johnson na ilihali Zanzibar wanatumia chanjo kutoka China (naomba kusahihishwa kama ni uongo).

Je, mbona hatusikii tena vifo, au wagonjwa wa COVID-19 katika nchi ya China ? Ina mana chanjo yao ni "effective" sana kuliko nyingine?

Ni hayo tu.
 
Ni kwanini sisi watanzania tutumie chanjo Ya Johnson & Johnson na ilihali Zanzibar wanatumia chanjo kutoka China(naomba kusahihishwa kama ni uongo)

Je mbona hatusikii tena vifo, au wagonjwa wa COVID - 19 katika nchi ya China ? Ina mana chanjo yao ni "effective" sana kuliko nyingine?

Ni hayo tu.

Chanjo unazoziona Tanzania ni misaada kutoka ughaibuni...

Tanzania bara imepokea msaada wa chanjo ya J&J kutoka Marekani chini ya mpango wa Covax...
Tanzania visiwani iliwahi zaidi kupokea chanjo iitwayo Sinovac kutoka Uchina, na sasa wameongezewa tena mzigo mwingine...

Huko China na kwingineko sio ya kwamba hakuna tena vifo, bali ile kasi ya vifo ilifanikiwa kupungua ingawaje idadi imeanza kuongezeka japo kwa uchache baada ya hiki kitu kinaitwa wimbi la 3
 
wagonjwa wa;
1.KISUKARI
2.UKIMWI
3.SARATANI
4.MOYO
5.PRESHA
6.TB
tuchukue tahadhari maaana hili wimbi la 3 la delta linapuputisha sana wenye maradhi hayo.
chukua tahadhari piga chanjo
 
Shukran kwa majibu mazuri mkuu mana nlikua najiuliza, tanzania iliundwa baada ya muunganiko wa tanganyika na zanzibar,, sasa nilitegemea chanjo tuchome za aina moja.

Zanzibar si unajua ile ni mamlaka kamili kwenye baadhi ya mambo ingawaje wao wana faida moja, bado wanaweza kunufaika na mpango wa Covax ambao serikali ya JMT inanufaika...(chanjo za bure)
 
Back
Top Bottom