Nina maswali kuhusu gari za umeme

Hiyo inaweza kuwa poa. Maana systems ya Battery iwe inachajiwa na systems ya umeme wa gari. Yaani Battery na umeme,viwe vinabadirishana moto kwa kuzunguka
 
No motor ipo wacha nikuoneshe uone motor ilivyo mounted!

Naomba msome post no 22 ya The Boss, mtaona msingi wa maswali yangu ulipoanzia.

Naelewa gari au chombo kinahitaji chanzo cha nishati ya mwendo ili kiweze kusogea. Sasa niliposikia hakuna injini wala motor ndio nikauliza hilo swali.

Nafikiri nimeeleweka
 
Ofcourse kama hizi petrol stations za bongo watatengeneza charging stations itarahisisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Bado itacoast kwenye muda. Maana sio sawa na mafuta unaweza kusimama kituo cha mafuta kujaza full kwa dakika hata 10. Lakini kujaza hilo kwa umeme muda wake sasa
 
Bado itacoast kwenye muda. Maana sio sawa na mafuta unaweza kusimama kituo cha mafuta kujaza full kwa dakika hata 10. Lakini kujaza hilo kwa umeme muda wake sasa
Ndo maana wanapambana kupata battery ambayo itachajiwa kwa muda mfupi zaidi na idumu kwa mile nyingi per charge!
Toyota anahangaikia Solid state battery huku tesla nae anaangaika na LPF batteries!
 
How can you run the motor?

I know and in fact understand that motor requires electricity to function.
Sasa kifaa gani utatumia cha kuzalisha umeme mbali na hivyo?
Kuna umeme unazalishwa bila kutumia solar wala gas (petrol au diesel). Sumaku zinapangwa vizuri kusababisha mzunguko unaozungusha kifaa cha kufua umeme. Ndio maana nikauliza consumption wa magari ya umeme specification ( power rating) ni zipi?
Ili umeme unaozalishwa hapo utumike na hiyo gari badala ya kutegemea battery zinazoisha nguvu baada ya muda na kuhitaji kupata cherge tena.
 
Kwahio hizo sumaku zitazalisha umeme continously bila kupoteza conductivity? Can i get a demonstration?
 
Kwahio hizo sumaku zitazalisha umeme continously bila kupoteza conductivity? Can i get a demonstration?

Ntakualika twende wote mkuu. Nimeona una interest na haya mambo, ntakupeleka ukashuhudie. Sio umeme tu, huo mzunguko unaweza kutumia kuendesha kitu chochote, hata pump ya maji.
 
Nina vifaa vingi vya zaman vina option ya ku switch kati ya 110 to 240v
 
Battery inapimwa kwa unit mbili.
Current na Time. Yaani ampere hour (N)

Kwa hiyo Unit kWh. ni unit ya electric energy.
Kuna namna ulitakiwa uulize swali na pia uzitaje some parameters ndio upate jibu
Kwenye battery za magari ndivyo wanaandika battery kwa hivo kwa watts yani kama ni nyingi sana ndo wanaandika kwh...battery za e car haziko rated mfano et 70v 50ah...hizo volt na ampia hata hazimuhusu mteja....wanapiga tu hesabu ya total watts inaadikwa hata power bank za kisasa hawaandiki eg 3.7v 20000mah badala yake wanandika total watts kama ni 70wh basi
 
Sio kweli mkuu nimeona nissan leaf anayo bi mkubwa fuu inakata unit 14 , na imejengewa banda na mita yak inajite
Sasa kwan hio leaf ya bi mkubwa ina battery ya 100kwh??

Battery ya 100kwh itajaa kwa unit 100 na kidogo kwa ajili ya upotevu wa umeme during charging and discharging
 
Naona pepo la free energy limekuingia ...ok unataka zalisha huo umeme kwa njia gani??
 
Kuna mzee mmoja mkazi wa Kawe yupo kwenye Youtube Channel ya Milard Ayo niliona anatengeza Kifaa kinachofua Umeme kwa kutumia Sumaku pekee,,,, ila hakueleza jinsi anavyopata mzunguko kwa kuzalisha umeme..
 
Kuna mzee mmoja mkazi wa Kawe yupo kwenye Youtube Channel ya Milard Ayo niliona anatengeza Kifaa kinachofua Umeme kwa kutumia Sumaku pekee,,,, ila hakueleza jinsi anavyopata mzunguko kwa kuzalisha umeme..

Ni kupitia huyo mzee na baada ya kumuona kwenye TV sikuishia hapo, nilimtafuta tukaongea nae kwa kirefu sana na kuona baadhi ya kazi zake.

Kwa ufupi tulifikia pazuri sana ila kuna mambo yakatokea ambayo sio vizuri kuyaweka hapa, yamemvurugia sana plan zake na hayupo tena kwa sasa. Hapatikani.
 
Sio kweli mkuu nimeona nissan leaf anayo bi mkubwa fuu inakata unit 14 , na imejengewa banda na mita yak inajitegemea
Mkuu za kutwa, nna ndoto ya kuagiza hiyo gari, nataka kufahamu TRA walimpiga kiasi gani kwa nissan leaf ya mwaka gani, ule mfumo wa tra hauna sehemu ya ku calculate kodi za gari za umeme pia email hawajibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…