Nina miaka 16 tangu nianze kufuatilia soka lakini swali hili limenichanganya

Nina miaka 16 tangu nianze kufuatilia soka lakini swali hili limenichanganya

Msela Wa Kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2021
Posts
1,396
Reaction score
2,704
Habari za mwamko waungwana,

nimejiuliza hili swali nikashindwa kupata majibu.

Kwa mfano timu A inacheza na timu B, Timu A wakapata penati, mchezaji wao akaipiga na kipa wa timu B akaitema mpira ukarudi uwanjani na kumkuta mchezaji mmojawapo wa timu A akafunga.

Je, hilo bao litahesabiwa kuwa ni la penati?
 
Hapana. Ni goli la kawaida tu.

Penalt inapotokea katikati ya mchezo ikipigwa hapo ndipo mwisho wake, na lile goli haliitwi la penalt hata kama lilienda direct golini.

Ni penalt za matuta baada ya kukosa mshindi tu ndizo magoli yake huitwa ya penalt.

Maana huwezi kusema leo Yanga imekuwa mshindi baada ya kuifunga Simba goli 5 kwa 4 ilhali magoli yote yalifungwa wakati wa mikwaju ya penalt.
 
Harafu Tena mpira wa kurusha ,mfano mpira ikatoka nje ukawa mpira wa kurusha ,mchezaji akarusha mpira Hadi golini vip Hilo linakuwa goli au ?
Hapana haitahesabika goli bali wataihesabu kama goal kick
 
Hapana, penalt ni ile kick ya kwenye kisahani
Habari za mwamko waungwana,

nimejiuliza hili swali nikashindwa kupata majibu.

Kwa mfano timu A inacheza na timu B, Timu A wakapata penati, mchezaji wao akaipiga na kipa wa timu B akaitema mpira ukarudi uwanjani na kumkuta mchezaji mmojawapo wa timu A akafunga.

Je, hilo bao litahesabiwa kuwa ni la penati?
 
Kipindi Cha nyuma kulikua na inderect kick, je kipindi hiki Bado ipo?
 
Harafu Tena mpira wa kurusha ,mfano mpira ikatoka nje ukawa mpira wa kurusha ,mchezaji akarusha mpira Hadi golini vip Hilo linakuwa goli au ?
Nawewe unamiaka mingapi unafuatilia mpira wa miguu?
 
Ni goli la kawaida. Niliwahi kubeti how next goal will bd scored-nikaweka kicking.
Ikatokea scenario uliyosema, mkeka ukaWIN. Ima maana goli halikuhesabiwa kama la penalt.
 
Back
Top Bottom