Nina miaka 19 nasumbuliwa na tatizo la kifua na vidonda vya tumbo. Nitumie mitishamba ipi?

Sikio la muazini

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2026
Posts
262
Reaction score
519
Msaada wenu wakuu tafadharini

Mimi ni kijana umri miaka 19 nasumbuliwa na tatizo la kifua na vidonda vya tumbo nilipima mara ya kwanza nikapewa dawa zikawa hazijanisaidia nikapima tena wapi?

Dawa nimemeza sana haipiti wiki nameza dawa leo usiku cjalala kifua na tumbo vinauma sana kwa pamoja na moyo" kwenda mbio na kizunguzungu mpaka muda huu ninaoandika tumbo bado linauma pamoja na kifua na moyo...!

Nahitaji msaada kwa ambae anajua dawa za miti shamba, maana dawa za kisasa nimetumia sana sijapata nafuu
 
Pole sana mkuu kwa maumivu unayopitia.

Kama umepima kwenye kituo kimoja tu , ningekushauri uende hospitali kubwa zaidi kama ya rufaa au ya mkoa, ukifika kwa daktari mueleze dawa ambazo umeshatumia na hazijakusaidia, kwa hiyo unaomba ufanyiwe uchunguzi mwingine wa kina.

Naamini utapata msaada Mkuu.
 
Ahsante.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…