Nimejaribu kufuatilia namna unavyo respond kwenye baadhi ya comment za wanaokushauri nimegundua vitu vifuatavyo:-Ndugu mimi ndo naanza sina uzoefu aise je nikimpa akalipigisha kazi likaaribika alafu yeye akalala mbele mda wa kushinda mahakamani ntautoa wapi ndugu
Kama kweli umeamua kuingia kwenye biashara Watu wametoa mawazo mengi mazuri sana tu...yafanyie Kazi ondoa uoga kabisa.Mimi pamoja na mke wangu ni watumishi wa serikali tumekaa pamoja tumeshauliana tumeamua kuchukua mkopo wa mil 45 lakini tatizo tulilonalo hatuna idea yoyote ya biashara maana kazini tunaenda asubuhi na kurudi jioni. Japo mungu ametujalia tumeweza kujikwamua na kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya boko chasimba.
Shida yangu kwenu je ni biashara gani naweza kufanya ili tuweze kujipatia kipato cha ziada bila kuaribu utaratibu wa kazi maana ikifika tarehe 14 wote tunakuwa tumeishiwa tunabakia ndani kuangalia CD za kikorea na kijapani.
Mawazo niliyokuwa nayo ni÷
1. Ninunue daladala ya habiria.
2. Ninunue bodaboda 5
3. Ninunue bajaji mbili
4. Nifuge kuku wa nyama
Maana siwezi kuweka fixed account kwakuwa pesa yenyew ni ya mkopo ushauri wenu ndugu zangu lakini wazo la daladala ndo tumelipa kipau mbele kikubwa naomba kwa mwenyewe uzoefu na iyo biashara ya daladala anipe msaada kwa umakini maana makato ya miaka 5 sio powa kabisa
Umemwambia ukweli haswa...,ni yeye sasa kama kweli atakuwa serious afanye maamuzi sahihi.Nimejaribu kufuatilia namna unavyo respond kwenye baadhi ya comment za wanaokushauri nimegundua vitu vifuatavyo:-
1. Una uoga wa asili
2. Hauna uwezo wa kukabili changamoto
3. Umekulia mazingira ya wasomiwasomi wengi au
4. Umesoma sana
Nianze na namba 3 na 4, watu wengi waliokulia mazingira ya wasomi wasomi au waliosoma sana (hata degree ya kwanza ni kusoma sana pia) na mazingira hayo yakawa hayana hata mfanyabiashara au mjasiriamali tunakosa uzoefu wa kufanya kitu nje ya ajira.
Namba 1 na 2 vinaweza kuwa matokeo ya namba 3 na 4.
Mtu muoga anaogopa kuanza.
Mtu muoga anawaza hasara kwanza badala ya faida
Mtu muoga hataki usumbufu
Mtu muoga hataki kukosana na watu
Kwenye biashara hivyo vitu HAVIKWEPEKI!
Hakuna biashara isiyo na hasara
Hakuna biashara isiyo na changamoto
Hakuna biashara isiyo na usumbufu
Na biashara nyingi lazima kuna kutofautiana hata na mteja tu achilia mbali uliowaajiri
Ukishajihisi ni muoga wa kupoteza, muoga wa usumbufu, muoga wa kukosana na watu achana na biashara zinazohusisha watu kwasababu kwanza sio lazima kila mtu afanye biashara na wala si kila mmoja anaweza kufanya biashara
Ni kweli kabisa tunahitaji kuwa na kipato cha ziada ila kuna vitu havifanywi na kila mtu.
Ushauri wangu kwako
Kwasababu angalau mwenzetu unauwezo wa kupata mamilioni yote hayo, kuna uwekezaji ambao unaweza kufanya usio na usumbufu
Mimi huwa naamini uwekezaji ni tofauti kidogo na biashara japo vinashabihiana
Unaweza kufanya moja kati ya vifuatavyo:
1. Tafuta kampuni inayopata faida kanunue hisa huko
2. Tafuta eneo (sio lazima iwe dsm), jenga stoo (sijui ndo godown) ambapo wakulima watakuwa wanatunza mazao yao huko kwa kulipia ushuru
3. Nunua mashine ya kusaga na kukoboa weka kwenye hiyo stoo kupanua wigo wa mapato
Katika hivyo vitatu sio rahisi kuibiwa pesa kizembe, hazina stress, hazina purukushani wala hazikuhitaji kuwepo kila siku japo kwenye mashine hapo utahitajika kuweka ndugu yako au mtu unayemuamini atukuibia ila hatakuibia sana
True.Biashara yoyote inalipa provided mtaji ni wa kutosha na usimamizi ni imara, hayo mengine ni nyongeza. Penda kufanya kile roho yako inapenda, hatuwezi kufanya wote kitu kimoja. Mfano mimi napenda sana niwekeze kwenye kilimo siku pesa na nafasi itakaporuhusu.
Kwa wewe mkuu nimekusoma unapenda biashara ya daladala. Ni biashara nzuri ukifuata misingi yake. Tafuta msimamizi mzuri tena awe ndugu wa karibu na mwaminifu. Huyu atasimamia mahesabu (mfano konda). Mfanye awe sehemu ya mapato mnayoyapata sio kumtumikisha tu. Pia wakati biashara inaendelea jifunze ABC za magari ili ujue vitu kama service, route zenye faida etc
Mwisho ukubali faida na hasara ni sehemu ya biashara yako, kuna siku mambo yatakua mazuri sana na kuna siku hayatakua sawa.
NB: Usinunue gari bovu, litakuliza ujutie. Usitegemee daladala yako 100%. Fanya biashara unayoipenda mkuu
Koote huko nimezurula ila hili wazo ndo la kupumzika sasa.hapa ni uhakika hamna inzi.(big up anko kidevu)Fuga kuku
WA nyama
Na kuku wa kienyeji..
Ila unaweza Jenga nyumba na ukauza ni sure bussines kipindi hujaiuza unapangisha
Hapa elimu inahitajika kidogo Mkuu,...Watu wengi wanaofanya biashara wala hawafanyi au kukaa karibu na biashara zao muda wote.,,kwa hyo kwenda kazini,au kuwa bize kiasi ngani hakukufanyi uogope kufanya biashara.Wazo langu kubwa ni kuagiza gari ya biashara maana sina mda kabisa wa kufanya biashara nyingine maana kazini tukiingia asubuhi kutoka ni jioni kwahiyo nimejaribu kuangalia kama naweza kupata kidogo kitu cha kusogezea maisha yangu maana mshahara siku zote hautoshi ndugu je wew kwa kazi yangu ungenishauri nifanye kitu gani bila kuathiri utaratibu wa kazi .Maana naogopa biashara nyingine naona kuangukia pua kutokana na kukosa mda wa kusimamia
@kisumapaiMimi pamoja na mke wangu ni watumishi wa serikali tumekaa pamoja tumeshauliana tumeamua kuchukua mkopo wa mil 45 lakini tatizo tulilonalo hatuna idea yoyote ya biashara maana kazini tunaenda asubuhi na kurudi jioni. Japo mungu ametujalia tumeweza kujikwamua na kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya boko chasimba.
Shida yangu kwenu je ni biashara gani naweza kufanya ili tuweze kujipatia kipato cha ziada bila kuaribu utaratibu wa kazi maana ikifika tarehe 14 wote tunakuwa tumeishiwa tunabakia ndani kuangalia CD za kikorea na kijapani.
Mawazo niliyokuwa nayo ni÷
1. Ninunue daladala ya habiria.
2. Ninunue bodaboda 5
3. Ninunue bajaji mbili
4. Nifuge kuku wa nyama
Maana siwezi kuweka fixed account kwakuwa pesa yenyew ni ya mkopo ushauri wenu ndugu zangu lakini wazo la daladala ndo tumelipa kipau mbele kikubwa naomba kwa mwenyewe uzoefu na iyo biashara ya daladala anipe msaada kwa umakini maana makato ya miaka 5 sio powa kabisa
Nimesoma kwa makini post yako lakini hujanishauri nifanye kipi na kipi niache ndugu
Yaan ni yeye tu ,ushauri mzuri kila mahali,...kama kweli ataamua kuufanyia Kazi atafaidika.@kisumapai
Nimesoma kwa utulivu ulichokiandika na nimeona haya
1. Katika siku 30, Mshahara wako na mwenza wako unatosha kwa siku kadhaa (tarehe 14 huwa hamna fedha za kutosha).
2. Hamna uzoefu wa biashara.
3. Umesha shauriana na mwenza wako aina za biashara.
Kwa mtazamo wangu fedha igawanye katika namna hii;
1. Biashara A. Hii iwe biashara ambayo itakupatia pesa ya kusaidia kuwezesha matumizi ya familia yako ya kila siku. Hii biashara iwe na uwezo wa kuingiza pesa ambayo ukiichukua haiwezi kuathiri biashara yenyewe.
2. Biashara B. Hii iwe biashara inayoingiza pesa itakayokuwa inahifadhiwa kama kukuza mtaji wenu wa biashara. Hii biashara iwe na uwezo wa kuingiza pesa kwa mwezi angalau faida ya asilimia 30% ya mtaji ulio wekewa (baada ya kutoa garama zote).
3. Biashara C. Hii iwe biashara ambayo itaweza kuingiza faida ya angalau 50% ya mtaji kwa kipindi cha kuanzia miezi mitano hadi nane au mwaka na iwe biashara ambayo unaweza kurudisha faida uliopata na kuongeza kama mtaji na kuipanua biashara hiyo.
Sasa aina gani ya biashara itakua ni biashara A, B na C inategemeana na vitu hivi;
1. Eneo unaloishi au utakalo amua kufanyia biashara
2. Muda utakao kuwa katika usimamizi na uangalizi wa biashara
3. Ujuzi juu ya usimamizi wa biashara ama kuwepo mtu wa kuweza kuangalia taarifa za biashara yako na kuweza kujua mwelekeo wake na kuweza kukushauri nini cha kufanya (iwapo mwelekeo hasi unatokea)
4. Utayari wa kupoteza mtaji (aidha kiasi ama wote).
Biashara inamengi huwezi kuwekeza leo kesho upate faida zingatia hilo na pili kuna tofauti ya mauzo (au pato kutoka kwenye biashara) na faida ya biashara.