Nina Milioni 45, msaada wanaJF

Tatizo ni mambo ya uaminifu... Ila ukiweza azisha biashara ya kukopesha school fees.... Wazazi wengi wana changamoto ya kulipa ada kwa mkupuo, wengi wanamudu kulipa kidogo kidogo. Ukiweza kuanzisha wewe unalipa full school fees na mzazi analulipa wewe kidogo kidogo pamoja na interest.
 
Mtu anachukuaje mkopo mkubwa hivyo bila kuwa na plan ya kufanya?

Anyway let's say anazipata kwa njia nyingine ni ngumu kumshauri mtu kwa hela zote hizo bila kuwa engaged professionally mkuu
Nimeelewa, hiyo pesa ni nyingi.Anahitaji msaada wa weledi
 
Duh yaani mpaka mnachukua mkopo hauna hata idea ufanyie nini hauko siriazi mkuu..labda ungesema una idea fulani then umeleta hapa watu waboreshe lakini haiwezekani umechukua hela nyingi hivyo halafu unataka watu wengine wafikirie kwa niaba yako.
 
Ngumu sana kupandikiza plan kwa mtu ambaye hana plan, pambana tu mkuu
 
~Mtafute Ontario akupe mbinu za kuchoma umasikini kwa muda mfupi...kwa mtaji wa 3m ukazalisha 19m kwa miezi 3!!!mtafute hutajutia mkuu.
 
Mkuu fanya biashara ya dagaa kwa ajili ya chakula cha kuku,wanapatikana jijini mwanza na visiwa vyake vya karibu,soko lake la uhakika ni Dsm,Tunduma etc....Anza na mtaji wa 3M-5M then as time goes on unaongeza mtaji.

Nipo tayari kuwa business partner.
(Muda ninao mwingi tu)
 
1. Jenga vyumba vya wapangaji,
2. Chukua ml5 nunua machine 5 za kupukuchua mahindi tafuta vijana waingie vijijini mlimba na tanga kuendesha hzo mashine then walete malengo.
 
Kama bado unahangaika na wazo nicheki tuyajenge. Biashara nayofanya inaweza kukuingizia hata 1m hadi 1.5m kwa wiki bila chenga wala longolongo, na uwanja mpana tu(mutual inclusive market). Tena hautaingiza zote kwenye biashara. Nitafute mkuu huenda hautajutia.
 
Wekeza kwenye forex mzee ..hutokufa masikini mkuu ata kazi utaacha
 
Nimeipenda hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…