Wengi wamekushauri vizuri,issue za wanawake na biashara za kuzunguruka ni tatizo sana.
Kwanza ili utake kufanikiwa kwa hilo jaribu kumsikiliza na kumpa nafasi yeye ndie awe mwenye wazo kuu,ila kama wewe ndio utajifanya unawazo kuu basi itakufa muda sio mrefu.Chukua kama mawazi matatu ya kwake kisha lete humu uchambuliwe.
Unaweza kuwa na wazo la Duka la mtaani,yeye akawa na wazo jingine.
Ila kwa mtaji huo ni mkubwa sana.
Kuwa makini na wala usimtishe nakumkaripia,hapo atakuwa anafanya biashara kwa hofu na wala hamtofanikiwa.
Muwe tayari kwa changamoto za aina yoyote hapo ndio ukomavu wa akili unakuja.Unaweza kukuta mtajo wote unakufa,sasa ukifa unaweza kukuta ndoa inatetereka kama hampo makini,kwa mwenye Hekma na ndoto huo ni muda wa kukaa na kutathmini kwanini mtaji umekata namna hii,huo ndio utakuwa mwanzo wa kuzi face changamoto.Na akili usi iset ikaamini kwamba hiyo pesa au huo mtaji ndio maisha yako,Keep it kwenye biashara kisha relax usubiri changamoto.