Nina million 5, nishaurini nifanye biashara gani

kibali

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
504
Reaction score
425
Wakuu heshima mbele,naombeni msaada wa mawazo jamani,nina sh.million 5 nataka nizizungushe kny biashara ambayo haitanisumbua hasa kwenye uendeshaji kwani mimi ni mwajiriwa hivyo muda wangu utakuwa siyo full time kny hiyo biashara,naombeni mchango wenu wa mawazo tafadhali.Mbarikiwe saaaana
 
Dah yani hamna mtu alikusaidia mpaka sasa...nway mi nadhani ungenunua bajaji tu zinalipa pia
 

Hiyo 5m. ni pesa halali au umemwibia mwajiri wako?
 
haya ni marudio ya jana, kuna mwingine alianzisha topic ana milion 3 ameshauriwa icheki inamaelezo yote

nimeiona ndugu yangu na nimeisoma yote,naamini ile thread siyo mwisho wa new idea
 
Fungua biashara ya kuuza sigara au uza pipi tu...tehetehe tehe!
 
huna haja ya kuanzisha threat mpya ya kutaka mawazo.. hebu peruzi thread nyingine kuna mawazo mengi utapata huo. usiwe mvivu wa kusoma thread nyingine!!.
moderators heb unganisha threads zote zinazotafuta mawazo ya biashara ya kufanya!!
 
Mwana Hongera
Kabla yakufanya jambo lolote omba nakumshukuru Mungu wako kukuwezesha kiasi hicho cha Pesa, pia muombe Mungu akulinde
na uepukane vishawishi vibaya. then make a good plan on what to be doe on that amount of Cash.
 
2 m fanya M-pesa na 2m nyingine fanya Tigo pesa 1 m iwe kwa ajili ya pango baada miezi minne utakuwa umerudisha pesa yako mkuu changamkia dili tafuta sehemu zenye msongamano wa watu wengi kama tegeta au mwenge na meneo mengine yaliyokaa kihivyo mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…