Nina wasiwasi hao jamaa walikuwa wakinong'ona kiasi cha wewe kusikia walikuwa wanapitisha ujumbe. Kwanza, kama kweli alipewa tigo hakupewa ili awaeleze watu wengine. Pili kama alipewa tigo na akala, tunajuwaje kama yeye ndiye muomba na mla tigo. Inawezekana kabisa jamaa aliwaona mlipokuwa makiingia ukumbini na akajua ninyi ni wapenzi lakini hampendi kuonekana mle ndani kama ni wapenzi. Mlipoamua kwenda kukaa viti tofauti ikawa nafasi ya jamaa kutia chumvi kitumbua chenu. Si ajabu siku moja ukamkuta jamaa akivinjari na mpenzi wako baada ya wewe kumtema. Ushauri: Jiridhishe na hayo yaliyosemwa kwa kuchunguza wewe mwenyewe kwa mbinu zako kabla ya kufanya uamuzi hasi. Wasanii wapo kibao