Kwa taaluma ya utabibu Medical profession kuna njia za aina tofauti tofauti ambazo wazazi wawili wanaweza kuzitumia ili kupata mtoto wa kiume au wa kike.
Baada ya uchunguzi wa uhakika uliofanywa na wataalamu wa afya ya uzazi na mtoto ni kwamba, sasa wazazi wanauwezo wa kuchagua kuzaa mtoto wa jinsia waitakayo kwa takribani asilimia 80 kwa kutumia kalenda.
Ili wazazi waweze kupata mtoto wa jinsia waitakayo ni lazima kuzingatia mambo muhimu kabla ya kutafuta mtoto wa jinsia waitakayo (kike /kiume).
Baada ya tafiti za kitabibu Medical researches kufanyika imethibitisha kuwa njia ya upandikizaji wa mbegu ndio njia ya uhakika zaidi ukilinganisha na njia ya kalenda Menstrual calenda
Njia ya kutumia kalenda ni njia ambayo ina mafanikio katika kufanikisha kupata mtoto wa jinsia ya kike au ya kiume kwa kuzingatia hali kamilifu ya afya kwa wazazi wote wawili pamaoja na mazingatio ya muda husika wa kushiriki tendo la ndoa kwa nia ya kupata jinsia ya mtoto husika.
Mpendwa rafiki, kumbuka ya kuwa mwanaume huzalisha mbegu “XY” , ‘X’ ya kike na ‘Y’ ya kiume lakini mwanamke huzalisha mbegu *“XX”* yenye sifa ya uke pekee.
Mbegu *‘X’* ya mwanaume ikikutana na mbegu ya mwanamke *‘X’* hapo ni lazima mtoto atakaetungwa ni wa kike hata hivyo, mbegu *‘Y’* ya mwanaume ikikutana na mbegu *‘X’* ya mwanamke hapo ni lazima mtoto atakaetungwa awe wa kiume.
Mbegu *‘Y’* huwa si imara sana lakini mwendo kasi wake ni wa haraka sana ukilinganisha na mbegu *‘X’*, hivyo hazikudumu kwa muda mrefu na huweza kufa kirahisi.
Mbegu *‘X’* ni imara lakini mwendo wake ni taratibu sana wakati mbegu *‘Y’* ni dhaifu lakini mwendo kasi wake ni haraka sana.
Kwa mwenendo na sifa hizo, wazazi hawanabudi kwenda sambamba na kalenda ya hedhi ili kufanikisha kupata jinsia ya mtoto wamtakae.
Ni muhimu sana mwanamke kuzingatia mwenendo wa mzunguko wake wa hedhi ni wa aina gani, kwa maana ya kwamba wastani wa mzunguko wa hedhi ni siku *28* hivyo yai lake hutoka siku ya *14*. Kuna mzunguko mfupi wa siku *21* ambao yai lake hutoka siku ya *10*. Na wale wanawake wenye mzunguko mkubwa wa siku *36*, yai hutoka siku ya *18.*
NB: Kawaida yai hutoka katikati ya mzunguko wa hedhi ukilinganisha na mzunguko wa mwanamke husika.
Baada ya kutambua mzunguko wa hedhi pia wanatakiwa kufahamu sifa ya mbegu *‘X’* na mbegu *‘Y’*, kama tulivyokwisha kueleza hapo juu.
Je, ni siku zipi wazazi wanapaswa kushiriki tendo la ndoa ili kupata jinsia ya mtoto husika?
Baada ya wazazi wawili kufahamu sifa za mbegu za uzazi yaani mbegu X na Y kama tulivyokwisha elezea katika sehemu ya kwanza. Vile vile wanapaswa kuelewa ni siku gani hasa ya kushiriki tendo la ndoa ili kupata jinsia ya mtoto wamtakae.
Wazazi (wahusika) wanapaswi kushiriki tendo la ndoa siku mbili au tatu karibu na ya yai la mama la uzazi kutoka, hapo kutakuwa na uwezekano mkubwa sana wa kutungwa kwa mtoto wa kiume kwa vile mbegu Y husafiri kwa kasi zaidi hivyo ndio itakayotangulia kwa maana hiyo ile mbegu X itakuwa imeachwa na kasi ya mbegu Y kutokana na kasi yake ndogo.
Kwa sababu hiyo wazazi wanaohitaji mtoto wa kiume wanatakiwa kushiriki tendo la ndoa siku mbili au tatu kabla ya yai la mama kutoka.
Pia ikiwa wazazi watahitaji kupata mtoto wa kike watatakiwa kushiriki tendo la ndoa siku nyingi kabla ya kutolewa kwa yai la mama, kati ya siku ya 9, 10, 11 kabla ya siku inayotarajiwa kutoka kwa yai la mama.
Hilo ni muhimu kuzingatia kutokana na tabia ya mbegu X mwendo wake kuwa wa taratibu hivyo itaweza kudumu kwa siku hizo nyingi, huku mbegu Y itawahi kuharibiwa kutokana na kutangulia kwake kwa kasi hali ya kuwa si imara
Mkuu kumbuka ya kuwa hii kanuni si ya kudumu kutokana na mwili wa binadamu hubadilika mara kwa mara hivyo inapaswa kuzingatia mzunguko wa hedhi kwa umakini zaidi, hii ni kutokanana matokeo ya kitafiti.
Jambo kubwa la kuzingatia ni kujua siku sahihi ambayo yai la mama linatoka ili mbegu X na Y zikutane na yai la mama na kufanikisha utungwaji wa mimba. Endapo wazazi watakuwa na ndoto za kuwa na mtoto jinsia tofauti ni vyema wakafuata utaratibu huo ambao haugharimu chochote. Cha kuzingatia ni mzunguko wa mwanamke ni wa aina gani. Eidha mzunguko mrefu, wa kawaida au mfupi.
Na hapo ndipo huwashinda wanawake wengi na kupelekea kupata matokeo tofauti kabisa na walivyo tarajia, unakuta mzunguko wa mwanamke ni siku 28 lakini kumbe yeye anatumia kanuni ya mzunguko mfupi ambao ni siku 21.
NB: Ni muhimu sana siku za kushiriki tendo la ndoa kulinga na tabia za mbegu X na Y.
Takwimu zinaonesha kati ya watu 10 wanaotumia kanuni hii, watu 8 hufanikisha kupata jinsia ya mtoto wamtakae.