Nina Nguvukazi Ninaomba Mtaji 250000

Mackay

Member
Joined
May 27, 2016
Posts
47
Reaction score
33
Salaam wakuu wanaJf
Mimi ni mwanafunzi katika chuo Kikuu Ardhi, mwaka wa tatu.
nimekuja kwenu kuomba mtaji kwa ajili ya biashara ya kuuza na kupark na kusambaza mbogamboga na matunda,
nimeifanyia tathmini na kuona ni biashara ambayo inahitaji mtaji mdogo na inarudisha mtaji kwa haraka zaidi.
Ninatarajia kuifanya biashara hii katika wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam.
Ninaomba mtaji huo uwe katika A: mkopo ambao nitaurejesha kwa makubaliano baina yetu ukiwa na riba au pasi na riba,
nitakukabidhi vyeti vyangu vyote kwa kuwa ndiyo dhamana pekee niliyonayo.
B:unipatie mtaji niuzungushe nikulipe kutokana na faida nitakayopata kwa siku ama kwa wiki,
C: unisaidie kuanzisha biashara kisha niikuze na kuanza ya kwangu binafsi huku nikikuachia ile ya mwanzo kuwa yako.
Katika biashara hii nalenga wanajamii wanaonizunguka, watu katika mitandao ya kijamii na wapitaji pia.
Uaminifu wangu ni mkubwa.
Kama una wazo lolote nitalipokea na kwa Wenye nia tafadhali nisaidieni kujikwamua kiuchumi.
Ahsanteni.
 

Kijana unaonekana una moyo sana na kujikwamua! kwa wengi waliokuzunguka laki mbili na nusu haiwaingii akilini ya kwamba unaweza kuanza biashara na kukwamuka! lakini ukweli mtu anaweza kuanza na hata 10,000 kwa pale penye nia. ila haingii akilini kwani maandalizi ya shughuli yoyote ile huwa na gharama zaidi kuliko katika kuiendeleza kwake! hiyo inaweza kupelekea watu kuvunjika moyo wa kukusaidia kwa kuona kuwa pesa huenda ikaishia kwenye nauli na ukarudi kuomba zaidi! Je umejiandaaje kimahesabu na mengineyo ambayo yatakuwa kama ni vichangia mafanikio ya shughuli zako!
ungejaribu kufafanua ili uweze kupewa msaada! jaribu kuweka ambacho tayari unacho ( mfano: eneo la kilimo, utalima mwenyewe ama msaidizi wa bure, na kadhalika nyingine ambazo zinaambatana na shughuli iyo) na hizo laki mbili unusu umepangia kwa matumizi gani? Kumbuka sio lazima kutaja ni mboga gani ama kilimo gani!! ila onesha namba zitakazowashawishi watu kukusaidia kwa imani ya kuwa utafanikiwa. weka namba kama inawezekana! hiyo moja! cha pili kwa kufanya hivyo unaweza kukutana na wataalamu humu ambao pia watakushauri kama kuna jambo hujalifikiria katika mipango yako kwani kama ndio unaanza unaweza kutana na gharama ambazo wewe hujazitilia maanani katika mawazo yako ya kupanga kujikwamua. nakutakia kila lakheri kwa ujasirimali na mori ulionao.
 
Aisee sitaki kukuhukumu ila kuna soemthing off kwenye maelezo yako sidhani kama upo serious. Hivi ulishindwa kusave hata hela ya boom ili kuweza kupata huo mtaji kama ulikuwa na nia ya kweli? Hivi mwaka wa mwisho huwa hamuendi industrial training? Umeshindwa kupata yaani laki mbili na hamsini kabisa? Je katika maisha yako umeshawahi fanya biashara yeyote? Sikukatishi tamaa ila inaoenekana haupo serious. Hapo chuoni kwenu unasomea nini? Nikusaidie mbinu za kupata hiyo hela. Sababu ukiipata kwa mbinu zako mwenyewe kuna kitu utajifunza. Ila ukisubiri ya kupewa inawezekana ukabadilisha matumizi na kama kweli ungekuwa na nia ya dhati kwa level ya elimu uliyofikia ungepata tu hiyo laki mbili na hamsini.
 
sina mkopo. nimefutiwa na Heslb.
kuna thread ukipitia utaiona.
 
sina mkopo. nimefutiwa na Heslb.
kuna thread ukipitia utaiona.
Sasa ada unalipaje? Hebu weka link ya hiyo thread ya kufutiwa mkopo. Bado siamini kwamba umeshindwa kupata laki mbili na hamsini. Unayo maarifa umeyakalia. Unasoma degree gani hapo nikupe mbinu? Maana badala ya kukupa samaki nataka nikupe hints za kuvua samaki.
 
2017, B.A. Community and development studies
KWa hiyo mwakani mwaka wa nne? Hiyo Degree ya chuo gani tena? Mbona siyaelewi maelezo yako? Ngoja nikuache tu maana naona maelezo yako hayapo sawa.
 
Pole kwa masaibu. Skillis gani ambazo unazo mpaka sasa hivi? Mfano project writing? Computer applications? Data collection?
 
labda wameisahau.
Kweli nchi yetu bado kazi ipo!!
kijana nilikutumia ushauri ujieleze kwa mipango ya hizo pesa ukaona ni upuuzi! na kutumia muda wako kujitetea tu kupewa mtaji! sasa sijui nisemeje ila bado nakutakia kila la kheri kama ni kweli unahitaji pesa hizo kwa kujiendeleza
 
Tufanye joint venture npo tayar kama itakuwa ishu serious nakupataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…