[emoji268] *UFAHAMU UGONJWA WA ENDOMETRIOSIS* [emoji268]
[emoji298][emoji298]Endometriosis ni ugonjwa unaowapata wanawake ambao unaambatana na magonjwa ya mfumo wa homoni na mfumo wa kinga ya mwili, ambapo seli na tishu zinazotengeneza ukuta wa ndani wa uzazi (endometrium), zinajijenga na kukua nje ya tumbo la uzazi. Seli na tishu hukua na kujificha katika eneo la nyonga(pelvis), tumbo la chini(abnomen) na kwenye ovari na ni mara chache ugonjwa kusambaa kwenye viungo vingine zaidi ya nyonga.
[emoji298][emoji298]Endometriosis hutokea pale seli na tishu zinapojijenga nje ya tumbo la uzazi na seli hizo na tishu zinakuwa na tabia ya kawaida ya
kujijenga na kuongezeka unene, na kubomoka wakati wa mzunguko wa hedhi kama zile zilizojijenga ndani ya mfuko wa uzazi. Lakini tofauti ni kwamba seli hizi na tishu zilizobomoka na zilizo nje ya tumbo la uzazi, hazitaweza kutoka nje kama damu ya hedhi anayopata mwanamke mwanzo wa mzunguko mpya. Endapo tatizo hili litaathiri ovari, zaweza kusababisha uvimbe ( kwa kitaalamu unajulikana kama endometriomas). Tishu jirani na uvimbe nazo zaweza kuathirika na kupata kovu au tishu kushikamana isivyo kawaida. Hii huweza kupelekea hata kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai ya uzazi.
www.sangidaherbal.blogspot.com
Hakuna sababu zilizo thabiti kuonyesha ni nini hasa kinachosabisha ugonjwa huu, lakini zifuatazo ni sababu zinazoweza kusabisha ugonjwa huu:-
[emoji117]Sababu za kigenetiki
[emoji117]Matatizo katika mtiririko wa hedhi
[emoji117]Mfumo wa kinga wa mwili
[emoji117]Mfumo wa homoni kutokubalansi
[emoji117]Operesheni ya uzazi-
Dalili za ugonjwa wa Endometriosis.
[emoji298][emoji298]Maumivu- Hii ndio dalili iliyo kuu kwa wanawake wenye ugonjwa huu. Mwanamke asiye na tatizo hili huweza pia kupata maumivu wakati wa kuona siku zake za hedhi lakini maumivu hayo huwa siyo makali kama ya mwanamke aliye na ugonjwa huu. Maumivu haya yanaweza kuwa ya aina tofauti:-
[emoji117]Maumivu makali ya hedhi:
[emoji117]Maumivu wakati wa tendo la ndoa, ambayo ni makali na ni tofauti na maumivu ambayo mwanamke anaweza kupata pale anapoingiliwa na mwanaume anapoanza kufanya tendo la ndoa.
[emoji117]Maumivu ya muda mrefu ya chini ya mgongo pamoja na nyonga.
[emoji117]Maumivu ya tumbo.
[emoji117]Maumivu wakati wa kupata haja kubwa au haja ndogo, na hii hutokea wakati wa hedhi. Na pia ni mara chache sana mgonjwa anaweza kuona damu katika haja kubwa au ndogo.
[emoji298][emoji298]Ugumba-Mwanamama kukosa uwezo wa kupata mimba.
[emoji298][emoji298]Kuona damu ya hedhi katikati ya mzunguko-Endapo hali hii itajitokeza mara kwa mara ni vizuri kumuona daktari wako kwa ushauri zaidi.
[emoji298][emoji298]Matatizo ya mmeng’enyo- Matatizo haya huambatana na kuhara, kukosa choo, tumbo kujaa, kichefuchefu, na haya yote mara nyingi hutokea wakati mwanamke anapoona siku zake za hedhi .
Kwa ushauri na tiba za maradhi mbalimabali wasiliana nasi
www.sangidaherbal.blogspot.com
+255 655 821 550
Sulayman Sangida