Nina shida ya mawasiliano ya aina yoyote ya wasanii wafuatao

Nina shida ya mawasiliano ya aina yoyote ya wasanii wafuatao

MENEMENE TEKERI NA PERESI

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2022
Posts
5,392
Reaction score
14,646
Kufa tutakufa kikubwa kujiandaa ,Asalam aleykum wanajukwaa hiyo ni salamu kwenu.

Tafadhali nina shida na namba za simu au mawasiliano ya aina yoyote kwa wasanii wafuatao nahitaji ikiwa unazo namba zao ,naomba usisite kunisaidia maana Kuna mahali wanahitajika sana.

BONIPHACE MWAITEGE, BAHATI BUKUKU, ABY- ALPHA

Ndugu zanguni nimeaminika na serikali ya Kijiji pamoja na wanakijiji kuwa wanahitaji kuwaona hawa wasanii wakati wa mavuno wanahitaji hawa watu wawaimbie nyimbo zao wakiwa wanafurahia mavuno yao siku ya tarehe 08/08/2024 hivyo nimepewa hii kazi tafadhali nisaidieni hizi namba maana wanakijiji hawatanielewa ikiwa nitashindwa kuwaleta hawa watu.

Wenu katika ushereheshaji wa Kijiji cha mpitilu katika kata ya mnyankulu.

MENEMENE TEKERI NA PERESI
 
Tafuta milioni kumi, kakodi uwanja wa mpira wenye fensi, mziki dj na mwanasheria,

mtafute huyo bukuku na shusho waambie una milioni nne kwa kila mmoja wao waje wapige show utawagharamie usafiri na malazi.

Kiingilio pokea wewe na sadaka zote ambaye hana hela atoe gunia la mahindi au mpunga kama kiingilio

Utanishukuru baadae.
 
vipi umejifanya mjuaji sana hapo kijijini eh au wewe ndio mjini unakujua pek yako?
 
0753582739 Bon mwaitege jaribu hii kama bado ama tumia ni mda mrefu sija wasiliana nae
 
Sasa unanishauri mimi tena rafiki yangu una uhakika mpaka nawataka unahisi hivyo sijafanya rafiki ?
Nimemaliza kila kitu wamebaki wao kuja kuhangaika na maiki zangu
Tafuta milioni kumi, kakodi uwanja wa mpira wenye fensi, mziki dj na mwanasheria,

mtafute huyo bukuku na shusho waambie una milioni nne kwa kila mmoja wao waje wapige show utawagharamie usafiri na malazi.

Kiingilio pokea wewe na sadaka zote ambaye hana hela atoe gunia la mahindi au mpunga kama kiingilio

Utanishukuru baadae.
 
0753582739 Bon mwaitege jaribu hii kama bado ama tumia ni mda mrefu sija wasiliana nae
Hii nimepiga limepokea lijamaa Lina gusauti gwa kigugumizi gunasema niaje bablah nikakata simu nikajua kabisa huyu sio mtafutiwa kifo Bony mwaitege
 
vipi umejifanya mjuaji sana hapo kijijini eh au wewe ndio mjini unakujua pek yako?
Mimi ndiye think tank wa Kijiji maana ukiona tukio lolote lenye mganganyiko kitaifa ni lazima wanakijiji waje kupata maelezo kamili kutoka kwangu hii ni kutokana na vile nikilewaga najikuta nawapanga sana Mara nimesoma nchi za Scandinavia na hivi najua kifaransa ndiyo kabisa sikawiagi kupiga simu kwa jamaa yangu kujifanya naongea na Emmanuel Macron hivyo wametokea kuniamini sana na kuniogopa ongezea na heshima isiyomithirika bila kusahau wanajua Mimi ni mtoto wa mjini Kati Dasalam hivyo kwangu hawapindui Mama Mwana Kuna kingine mrembo wangu ?
 
Back
Top Bottom