Nina shida ya tatizo la Ngozi, naomba ushauri

Nina shida ya tatizo la Ngozi, naomba ushauri

June blizzard

Member
Joined
Aug 14, 2024
Posts
5
Reaction score
4
20240819_153601.jpg
Shida hii ipo usoni tu na ni baadhi ya sehemu ya uso, ni kama vidoti vyeupe na ilinianza toka 2022. Nimetumia dawa za Mba lakini wapi, nikaenda pharmacy wakaanza kunipa dawa za  Fungus zakupaka na kumeza. Nikaja kwenda Hospital nikapatiwa pia dawa zakumeza siku 30 na yakupaka.

Nimejikuta nimetumia dawa nyingi (vidonge na zakupaka) lakini bado hakuna matokeo chanya. Na vina zidi kuenea.

Mwaka huu nimeenda Hospital moja ina Specialist wa ngozi, nikaenda na list ya dawa ambazo nimeshatumia. Akaniambia kama umeshatumia dawa zote hizo na hakuna matokeo basi sio fungus. Shida itakuwa nini wakuu?
 
Hii inaitwa Vitiligo,ni tatizo la cell za ngozi kushindwa kuzalisha melanin kwa ufasaha.Tatizo hili hutibika haraka sana kama litashughulikiwa ndani ya miezi miwili ya mwanzo wa dalili.Kama utaendelea kutokupata nafuu unaweza kuniconsult.
 
Pole mkuu, mtoto wangu alipata tatizo kama lako japo yeye havikuwa vyeupe kun'gaa hivo. Nilipoenda nae kwa specialist wa ngozi alimpima choo na majibu yalipotoka akasema shida inaanzia huko tumboni. Akapewa dawa za kutumia na alipona havijarudia tena
 
Shukrani kwa ushauri wako🙏.
shida inakuja, hii hali ina miaka miwili sasa. Na vilikuwa vidogo tu lakini kadri siku zinavyozid kwenda mbele vinaongezeka.
Hii inaitwa Vitiligo,ni tatizo la cell za ngozi kushindwa kuzalisha melanin kwa ufasaha.Tatizo hili hutibika haraka sana kama litashughulikiwa ndani ya miezi miwili ya mwanzo wa dalili.Kama utaendelea kutokupata nafuu unaweza kuniconsul
 
Shukrani, labda ungenisaidia Kituo ulichoenda kupata matibabu na mimi niweze kwenda ,tafadhari.
Pole mkuu, mtoto wangu alipata tatizo kama lako japo yeye havikuwa vyeupe kun'gaa hivo. Nilipoenda nae kwa specialist wa ngozi alimpima choo na majibu yalipotoka akasema shida inaanzia huko tumboni. Akapewa dawa za kutumia na alipona havijarudia tena
 
Vitiligo hiyo muone dermatologist ila hiyo sura mbona imefanana na Afande Kingai.
Shukrani kwa ushauri japo nimeshaonana na specialist wa ngozi na alinipa maelekzo kama niliyoandika hapo juu.
😅Kuhusu Kufanana na afande, hapana sio mimi huyo.
 
Shukrani kwa ushauri wako🙏.
shida inakuja, hii hali ina miaka miwili sasa. Na vilikuwa vidogo tu lakini kadri siku zinavyozid kwenda mbele vinaongezeka.

Habari, pole kwa kuumwa.

Nakushauri ufuatilie ushauri hapo juu namba 3. Hili ni tatizo la mfumo wa kinga wa mwili bhifi ya seli zinazozalisha rangi nyeusi ya ngozi/malanini. Tatizo hili lina asili ya kurithi pia.

Kupigwa na mwanga wa jua moja kwa moja pia huchochea kuongezeka kwa tatizo. Wagonjwa hushauriwa kuvaa kofia pana ili kujikinga na hilo.

Matibabu yake ni mtambuka na yanahitaji ufatiliaji mzuri na uzingativu. Ongea vyema na mtoa huduma wako.
 
Msaada dawa gan ya kutumia ama dk mzuri wapi
 

Attachments

  • 1725046163149.jpg
    1725046163149.jpg
    109.5 KB · Views: 7
  • 1725046146057.jpg
    1725046146057.jpg
    90.8 KB · Views: 8
Back
Top Bottom