Nina tatizo la Gari Kutetemeka na Kuzima

Nina tatizo la Gari Kutetemeka na Kuzima

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Kwema Wakuu,

Za Weekend?

Gari yangu nilibadilisha Gasket last week, Sasa toka hapo imekua inatetemeka napokua nimesimama kwenye Mataa labda. Pia asubuhi nikiiwasha inawaka na kuzima. Mpaka nirudie rudie mara kadhaa ndio mwishoni litakubali.

Yaan nikiwasha linatetemeka na nikitia Gia labda ndo linazima. Hii inatokea hata jioni napokua nawasha pia. Ulaji wake wa mafuta pia umeongezeka kulingana na kabla sijabadili gasket.

Gari ni RAV4 Kili Time, shida inaweza kua nini hapa?
 
Nina assume ulibadilisha blown HG sababu gari ilikuwa inachemka..
Vitu vya kucheki na fundi wako..
Timing belt ilifungwa sawa..!!?
Vikombe aliviadjust..!!?
 
Nina assume ulibadilisha blown HG sababu gari ilikuwa inachemka..
Vitu vya kucheki na fundi wako..
Timing belt ilifungwa sawa..!!?
Vikombe aliviadjust..!!?
Ilichemsha mkuu,
Sijajua kuhusu vikombe na timing belt
 
Fundi wa chini ya muembe atakua kakupiga na kitu kizito....

Check na fundi mwingine na hakikisha kwenye matibabu wewe upo muda wote....

Wataalamu wataongezea nyama.
 
Ilishawahi kunikuta hiíi nikabadilisha mfuniko wa Rejeta tu gari ikawa mpyaaaaa hadi leo nakata mitaaaaa tu.

Badilisha na wewe ila isiweke wa bei rahisi weka ule wa 20k au 10k
Haiko related na mfuniko wa rejeta hii master. Mfuniko wa rejeta ile inatokana na engine kua inaoverheat ambapo at times inaeza pelekea hata hosepipe ile kufyatuka.

Kama gari bado inachemsha, kwanza unatakiwa utambuee hio gasket aloibadilisha ilikua ya aina gani, ya plastic ama ya chuma? Kama aliweka ya chuma itazidi kusumbua tu maana once gasket ikishabadilishwa kwa ishu ya kuchemsha always ukieka ya chuma itaendeleza tabia ile ile ya kuchemaha
 
Back
Top Bottom