Nina tatizo la kifafa, nini tiba yake?

Nina tatizo la kifafa, nini tiba yake?

Ubwa Juma Mpenja

New Member
Joined
Feb 24, 2019
Posts
1
Reaction score
2
Nina tatizo zaidi ya mwaka sasa huwa nadondoka na kukakamaa na povu likinitoka kama ninavyoelezewa na ndugu zangu.

Kama kuna anayejua dawa ya haya maradhi naomba anisaidie
 
Ulipoanza kupata hilo tatizo ulikuwa unaumwa kitu kingine?
Lazima kutakuwa na chanzo.

Je inakupata ukiwa katika hali gani. ...wakati unamsongo wa mawazo au wakati unaumwa au hata ukiwa mzima wa afya?

Ningekushauri umwone mtaalam, upatiwe vipimo na kupewa matibabu kama sio yakuponyesha basi hata yakukuwezesha kuhimili hiyo hali. ..isije kukuletea matatizo zaidi huko mbeleni
 
Hapa utakutana na wizi tu wa kukuuzia Mitishamba Fake (Tiba Asili).

Usitumie Dawa Yoyote:

√ Fanya Mazoezi kila siku
√ Changia Damu Mara kwa Mara (Kwa Timu ya Damu Salama).

Ukifanya hivyo lete mrejesho hapa

Yupo mmoja alikaribia kushindwa Kufanya Mtihani wa Form Four kwa tatizo kama lako.

Baada ya Kufanya kama nilivyokwambia Wewe Amefanya Mtihani wa F4 akaingia Kidato cha 6 na sasa yupo UDOM amepona kabisa bila ya kuugua hata Siku moja.

Damu yako ndio tatizo lako, Ipunguze kwa Mazoezi na Kutoa Mara kwa Mara.
 
Back
Top Bottom