Nina Tsh. milioni 16, nataka kununua Hiace nifanye biashara ya daladala

Nina Tsh. milioni 16, nataka kununua Hiace nifanye biashara ya daladala

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,023
Wadau kichwa cha habari kinajieleza.

Naomba kujua wapi napata gari, faida na changamoto. Gari itakuwa mkoani

=====
Hongera boss kwa mtazamo huo chanya....
Ila naomba fikiria huu msemo wa WARREN BUFFET alisema "Be fearful when others are greedy and be greedy when others are fearful" huyu ni baba wa biashara uwekezaji duniani....
Liangalie kwa jicho la tatu hilo wazo lako
tathimin lini utaanza kupata faida ya kile ulichowekeza hapo...na risk zake zipi...na je namna ipi ya kupunguza hizo risk.?

Maana risk huwezi kukwepa kwenye biashara yoyote.... sema huwa tunazipunguza tu... kwamba hata risk ikitokea iwe kidogo...yaan himilivu.

Zaidi sana if you are opened mind enough... Njoo pm tujadili biashara ya kufanya pamoja...as joint Company. Uhakika wa faida ya 10% kupata kila mwezi kwa huo mtaji upo.ni mikakati na mipango tu...

Fikiria 10% faida ya mill 16 kila mwezi na mtaji wetu unabaki salama. Wewe unakuwa msimamizi Mkuu wa mahesabu ya biashara...faida kila mwezi tunagawana au itategemea na makubaliano yetu.

Sheria na taratibu zote zitafatwe kufikia makubaliano ya pamoja ili kila mtu ajiridhishe.
Karibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na mawazo ya kununua gari kwa hele hiyo utajiongezea umaskini, labda ununue hiyo hiace mpya mill 32 ndio utaona hela yako inarudi, ukinunua kwa mtu umekwisha.

Otherwise nunua bajaji 2 zitakutoa.
Wadau kichwa cha habari kinajieleza...
Naomba kujua wapi napata gari,faida na changamoto...
Gari itakuwa mkoani

Miller = Milioni(pesa)
Tzs

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usijaribu kitu kilicho tumika Bongo!... usijaribu kumvua mtuu .. jichange uagize Japan
 
Nakushauri kuwa uachane na biashara ya Hiace. Utakuja kujuta. Hiyo hela wekeza hata kwenye kiwanja au uiweke Benki kwenye akaunti ya fixed deposit. Ukinunua Hiace umewanunulia wafanyakazi wa kuisimamia ili wafaidike.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wadau kichwa cha habari kinajieleza...
Naomba kujua wapi napata gari,faida na changamoto...
Gari itakuwa mkoani

Miller = Milioni(pesa)
Tzs

Sent using Jamii Forums mobile app

Nachojua mimi hiace used kutoka Japan ni kuanzia milioni 25 sasa hiyo milioni 16 sijui unataka kununua hiace ya kupiga nayo picha ikiwa juu ya magogo ili wanao waseme baba alikuwa na gari


Sent using IPhone X
 
Back
Top Bottom