Nina Tsh. milioni 16, nataka kununua Hiace nifanye biashara ya daladala

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,023
Wadau kichwa cha habari kinajieleza.

Naomba kujua wapi napata gari, faida na changamoto. Gari itakuwa mkoani

=====
 
Achana na mawazo ya kununua gari kwa hele hiyo utajiongezea umaskini, labda ununue hiyo hiace mpya mill 32 ndio utaona hela yako inarudi, ukinunua kwa mtu umekwisha.

Otherwise nunua bajaji 2 zitakutoa.
Wadau kichwa cha habari kinajieleza...
Naomba kujua wapi napata gari,faida na changamoto...
Gari itakuwa mkoani

Miller = Milioni(pesa)
Tzs

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usijaribu kitu kilicho tumika Bongo!... usijaribu kumvua mtuu .. jichange uagize Japan
 
Nakushauri kuwa uachane na biashara ya Hiace. Utakuja kujuta. Hiyo hela wekeza hata kwenye kiwanja au uiweke Benki kwenye akaunti ya fixed deposit. Ukinunua Hiace umewanunulia wafanyakazi wa kuisimamia ili wafaidike.
 
Reactions: BAK
Wadau kichwa cha habari kinajieleza...
Naomba kujua wapi napata gari,faida na changamoto...
Gari itakuwa mkoani

Miller = Milioni(pesa)
Tzs

Sent using Jamii Forums mobile app

Nachojua mimi hiace used kutoka Japan ni kuanzia milioni 25 sasa hiyo milioni 16 sijui unataka kununua hiace ya kupiga nayo picha ikiwa juu ya magogo ili wanao waseme baba alikuwa na gari


Sent using IPhone X
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…