Nina uhahika 98% hawajui hili

Amafita

Senior Member
Joined
Jul 22, 2019
Posts
165
Reaction score
311
Habari wa JamiiForum.

Najua imezoeleka katika jamii zetu kwa rika zote (watoto, vijana, wazazi na hata wazee) aidha wasomi au wasio wasomi kutumia neno Nimekumiss pale unapomaanisha kumkumbuka mtu hasa uwepo wake. Hata hivyo neno mbadala la kiswahili ni Kupeza hivyo basi unaweza ukwamwambia mpendwa wako kuwa Nimekupeza
 
Hii ndo mada sasa cz inafundisha na kukuza lugha yetu adim KISWAHILI nice[emoji106]
 
Sikuwahi kulisikia, leo ndio mara ya kwanza
 
Naanza na mwandishi..... Nimekupeza....
 
Nimekupeza
 
Hapa napata mkanganyiko kidogo ipi ni sahihi " adim " au " adhimu " kwa anayefahamu
Yote ni maneno ila neno adim lilitakiwa liandikwe adimu. Kwa kifupi maneno yote ni ya kiswahili na yana maana mbili tofauti japo watu wengi hudhani yote yana maana moja ila sivyo
 
Sio uongo na usikimbilie kukosoa pasipo kujua. Naona umesimamia ile dhana ya Direct translation ila kwa neno hilo umechemsha. Ukisema "nimekukosa" unahamisha maana kabisa yani ni sawa na Waganda wanavyohangaika kila kukicha kufanya utafsiri wa moja kwa moja kwa maneno ya kiswahili wasioyajua. Mfano ni huu,kasikilize wimbo unaitwa "Na wewe" ulioimbwa na Cindy Sanyu wa Uganda ndio utaelewa ninachokwambia
acha uongo mkuu,, NIMEKUMISS=NIMEKUKOSA
 
Nimekupeza Lovenear
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…