Nina uhusiano na mwanamke wa 28 miaka 28 lakini kaolewa na mzee

kitu cha kwanza uzinzi ni dhambi, ikimbie zinaa haitakuacha salama. pili, wazee ni viumbe wenye wivu mkubwa sana kwa wake zao hasa hao wanaosemekana hawajiwezi, majoirity huwa washapita sana kwa waganga, hakuna siyejua madawa. akigundua, mke huwa hamdhuru, ila wewe lazima akupige tukio. umri wako bado mdogo, angalia future yako, usione vichaa barabarani ukafikiri walizaliwa hivyo, wazee ni wabaya sana hasa kwenye suala hilo, na huwa wanaenda kimyakimya.
 
Mwambie aombe Taraka umuoe wewe. Aachane na uyo Babu.
 
Acha masihara na wake za watu ......acha aiseee.
 
Shwetani wewe ushindwe
 
Mkuu ww umemtongoza kabisa na akakwambia mzee ni mmewe lakini umekaza fuvu!

Mm demu wangu aliolewa na mzee tena kafanywa mke wa tatu

Cha ajabu ananambia bado anahisia namimi na mzee yupo bize, kwahiyo demu muda mwingi anaishi mwenyewe.

Mm nimemtema mazima na nimetimua mbio ndefu sitaki mazoea nae na cm zake niliblock.

Kaa nae mbali mkuu tamaa za hovyo hupelekea umauti au ulemavu wa kudumu.
 
Ukiwafahamu wanawake Wala huwezi kuja kuuliza hapa

Wanawake ni kawaida Yao hisia zimepungua Kwa mzee zimehamia kwako na wewe siku Moja zitahama zitakimbilia Kwa mwingine na huko alikokimbilia atakusema vivo hivo

Lakina fahamu mzee akikugundua unalo unaweza ukazikwa mzima akheri angekuwa kijana mwenzako ila Kwa mzee unalo
 
Bongo kuna ufala sana, sasa unataka ushauriwe kitu gani mkuu?? Unamgonga mke wa mwanaume mwenzako alafu unakuja kubana pua eti naumia naumia, mademu wapo kibao mitaani wewe tu na kamba zako
Hovyo kabisa!
 
Pesa si kila kitu, cc wazee wa "Tafuta hela" wanavyoukwepa huu uzi😁

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Siku mzee akikuomba ndogo ulete mrejesho
 
Anza kufumua marinda yako mwenyewe kwa kidole chako siku mzee akikukamatia akute yamefumuliwa kabisa.

Unadhani wazee hawana wivu na sio wanaume rijali
 
Kijana wangu nikikwambiaga una ulemavu wa akili unaona kama nakitukana unakula mke wa mtu alafu unakuja kuomba ushauri hapa
 
Jipige kifua mara 3 kisha sema kwa sauti "mimi ni mshenzi"

Huwezi kutembea na mke wa mtu halafu ujifanye kumuhurumia mwenye mke. Huruma ingeanza kabla hujamtongoza
 
Wewe siku zako za kuomba maji ziko karibu sana.
 
Sawa,wewe endelea mzee hana noma. Ila baadae hatutaki kuambiwa kwanini hatukupazii sauti kwa kufanyiwa unyama na Maafande πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…