Nina ujauzito, tatizo langu mguu wa kulia unaniuma sana

Evz

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
674
Reaction score
130
Tangu mwezi wa pili mpaka leo nina ujauzito wa miezi 8. Mguu wangu wa kulia unaniuma sana.

Je? nitumie dawa gani au dalili gani hizi?

Msaada jaman napata tabu.
 
tangu mwezi wa pili mpaka leo nina ujauzito wa miezi8. Mguu wangu wa kulia unaniuma sana. Je? Nitumie gani au dalili gani hizi? Msaada jaman napata tabu.

umetembelea clinic? Hawajakupa ushauri wowote?
 
Tangu mwezi wa pili mpaka leo nina ujauzito wa miezi8. Mguu wangu wa kulia unaniuma sana. Je? Nitumie gani au dalili gani hizi? Msaada jaman napata tabu.
Badala ya wewe kwenda kwanza Hospitali unataka ushauri wa watu humu ndani? pole sana bibie tafuta Mafuta ya karafuu uchanganye na mafuta ya Zaituni uwe unajipiga masaji kila siku asubuhi na usiku utapona inshallah. Uguwa pole bibie utajifunguwa mtoto kiume inshallah Evz

mmm mwite MziziMkavu. atakusaidia tatizo lako
Ndugu a.rahabu hujambo wewe lakini? ukiwasaidia hawa ndugu zetu wakipona hawaji kusema kuwa wamepona au bado watakuja kulalamika dawa unayowapa imewaletea madhara ndio binadamu jinsi alivyo tunapenda kukosoana kuliko kutoa shukrani. MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO.
 
Tangu mwezi wa pili mpaka leo nina ujauzito wa miezi8. Mguu wangu wa kulia unaniuma sana. Je? Nitumie gani au dalili gani hizi? Msaada jaman napata tabu.

Kitu cha kwanza muhimu sana ni kupimwa ili kuhakikisha kuwa hakuna damu iliyoganga kwenye huo mguu.

Iwapo hakuna damu iliyoganda basi maumivu yanaweza kuwa yamesababishwa na uzito uliopo tumboni kulalia mshipa wa fahamu. Tatizo la namna hii huisha baada ya kujifungua.

Ni vizuri pia ukapimwa sukari mwilini.

Kumbuka, maumivu yanaweza kusababishwa na matatizo mengine yasiyohusiana na ujauzito.

Fika kwenye kituo cha matibabu ili upimwe na kupewa ushauri maalum kulingana na hali yako.
 
asanten kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…