Nina uvimbe kwenye korodani. Niende hospitali gani hapa Dar?

G O G

New Member
Joined
Nov 27, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Habari za mida Wana jamii, Mimi ni kijana Nina umri wa miaka 29 miezi mitatu iliopita nilijigundua kua Nina uvimbe kwenye korodani kutokana na maumivu ya hapa na pale ndo kujichunguza nikagundua tatizo.

Nikaenda kwenye hospitali huzi zinazotibu magonjwa yasioambukiza nimemaliza dozi ila sijaona kupungua mana nilipewa dawa za kuondoa uvimbe bila upasuaji sasa nimekuja kwenu ndugu zangu nisaidie niende hospitali gani hapa mjini nikatibiwe?
 

Pole kwa kuumwa.
Unahitaji kumwona daktari ili apate historia ya ugonjwa wako vyema, akuangalie tatizo husika/examination na pia vipimo hasa itakapohitajika. Ni vyema kituo/sehemu husika kuwa na uwezo wa kufanya ultrasound ya eneo husika.

Hospitali zenye hadhi ya mkoa au rufaa zina uwezo wa kufanya vyema kwenye tatizo husika.
 
Tafuta hospitali yenye Urologist.Wacha kwenda kwenye zahanati ndogo na kupewa dawa bila vipimo sahihi.
 
Asante sana ndugu zangu Kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…