Mimi nimeagiza Gari kabla sjiampa Dereva nikaamua Nianze kuliendesha Mwenyewe Kwanza Kama dereva na Mmliki pia.
Nimejaribu kufata Hints zao vizuri ikiwemo kuingia barabarani mida ambayo Demand ni kubwa na pia Maeneo potential kama city center, Maeneo kama mlimani city, Upanga,Mwenge,Koko,Masaki,Kurasini(Uhasibu/Kota Bandari)
Kwakweli biashara ni ngumu. You can imagine siku nzima napata wateja wa tatu.Mara wawili, Na bei ni kama mnavofaham zipo chini sana.
Nimewahi kumtoa mtu Baruti mpaka Tabata segerea ndani ndani offroad. Usiku bei ikaja Elf12 na barabara ni mbaya hatare.
Kkoo kurasini Sh 3000
Baruti - Mawasiliano tower. Law school Sh 4000
Mind you kuna wakati unapaki mahali 2hrs hujapata request.Unaamua kubadili location.kwa Garama zako. Na huko uendako huna uhakika wa mteja pia. Au ndo ukapata wale wa 3000. Au mara ukakutana na mtu anaoffer.
Kuna siku asubuhi nimeweka mafuta ya 20k. Mpaka usiku wa saa nne. Nimepata sh 15 tu. Hata ile 20k yangu haikurudi.
Kuifupi hii mimi nimeona ni biashara kichaa. Anaefaidika nu Taxify na Mteja. Dereva na mmiliki hali ni tete kwa sasa ivi.
Kama una Gari Taxify/Uber unaletewa hesabu vizuri nakushauri kakague Gari lako.