rushanju
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 3,238
- 5,106
mimi nina wasiwasi na chanjo hizi ingawa sio daktari. Ninaomba ushauri wakina kutoka kwa wenye ujuzi hasa suala la chanjo hizi mpya za kichomi na kuhara. Ninachojua ni kwamba kuhara ni hali ya mwili kutaka kujisafisha hasa pale mtu anapokuwa kapata maabukizo katika njia ya chakula. Kuharisha usahidia sana kupunguza sumu au bakteria ambao watakuwa wameingia tumboni. Nauliza hii chanjo itakuwa msaada au kero? Mi niniachojua nikwamba magonjwa yote yenye chanjo mtu akiugua huwa ni maramoja kama ukipona huwezi kuupata tena ugonjwa huo. Je? Mtu anaweza kuharisha na hasiharishe tena maishani? Au kichomi huja mara moja tu? Jamani naomba ushauri.