Nina Wasi Wasi na Tenda za Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Hivi karibuni wizara tajwa hapo juu wametangaza vijitenda vya ku supply vitu mbali mbali. Lakini mashariti magumu yaliyowekwa kwa mshiriki, kuna nitia wasiwasi kuwa kumefanywa kwa makusudi ili vikampuni vya wazawa ambavyo havijakidhi mashariti hayo visiweze kushiriki na kuwapa nafasi makampuni yao yaliyopakwa mafuta kuweza kubaki machache na kubid kwa bei watakazo penda wao!

Hembu tuanze kuchambua masharti waliyoyaweka tuone kama ni fair kwa makampuni madogo ya kizalendo:

Tenda iliyotokea kwenye gazeti la Daily News la tar12 March 215 Lot no 3 inahusu kusupply fire extinguisher 40 ambazo hata kila moja ikiuzwa laki moja moja, itagharimu shilingi milioni nne tu kusupply fire extinguisher. Lot no 5 inahusu kusupply ngazi 40. Ambazo hata ngazi moja ikiuzwa kwa shilingi laki moja moja, itagharimu milioni nne tu kununua ngazi hizo...

Mashariti kwa kampuni kukidhi vigezo
1.Kwanza kununua tenda sh laki moja
2. Mshindani wa zabuni lazima awasilishe financial statements ambazo zimekaguliwa (audited) za miaka mitatu,
3. Uzoefu wa miaka miwili wa kutoa huduma kama hiyo,
4. Dhamana ya tenda (bid security) ya asilimia 2.5 n.k

Kwa hiyo unaweza ona, kikazi ambacho hata ngosha alitakiwa akifanye kupeleka watoto wake chooni kimewekewa kiwingu ili tu kumuengua mtoto wa mkulima na kuwapigia chepuo wajanja wachache ili wapate ulaji.

ILANI
Ilani yangu ni kuwa katibu mkuu wa wizara asitishe tenda hii ili itangazwe upywa na kwa mashariti nafuu. Mashariti waliyoweka ni kwa tenda kubwa kubwa kama za bara bara, au za miradi ya umeme ya mabilioni na sio ya vikazi vidogo vidogo vya kufanyw na mtoto wa mkulima...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…