Nina wasiwasi na hivi vyeo jamani

Nina wasiwasi na hivi vyeo jamani

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Jamani nimesoma gazeti moja jana likilalamika sana utoaji wa vyeo vya polisi/jeshini

kutokana na hali ya hewa hivi sasa yawezekana vyeo vinatolewa kwa mtu wa darsa la saba...na wewe umengia na form four/six unamsikia mwenzio kwenye bomba...kama tulivyosikia na vyuo vyetu vimeanza kutoa degree za uongo...na kufikia mawaziri wetu tuliowaita majina ya ""DK" kwa miaaka nenda rudi kuamua kurudi darasani upya kusomea udaktari

....sasa mi nimewiwa na hivi vyeo vya sijui CAPT CHILLIGATI...LTN MAKAMBA..CAPT AGRREY.M...NA WENGINEO...YAWEZEKANA WAMEPATA HIVI VYEO KIFISADI NINGEOMBA KAMA WAHUSIKA WANAWEZA KUCHUNGUZWA WALIVYOPATA VYEO VYAO NASI TUKAJIRIDHISHA UFISADI WA VYEO NI VYUONI TU NA SIO JESHINI AMA JESHI LA POLISI......KUNA WENGI TU WANAJIITA KANAL..LTN KANAL..TUWACHUNGUZE HAWA YAWEZEKANA KABISA AWAKUTAKIWA KUITWA CAPT CILIGATI,,CAPT AGGREY..LTN MAKAMBA......

ANGALIENI MSIGUSE CHA MKULU NASIKIA NA YEYE NI LTN KANAL...MMMHH

WANANDUGU TUSIKASIRIKE HII YOTE NI KUJIRIDHISHA TU NA VIONGOZI WETU KAMA YALIOWAKUTA MAWAZIRI WETU........
 
Mama mia inapendeza kuona kuwa baada ya kuumwa na nyoka sasa ukiona ujani unashituka.

Kifupi hawa wakuu ni kweli wana hizo hadhi/vyeo na walivipatia Tanzania Military Academy (TMA monduli) monduli enzi hizo ilikuwa inaitwa CTU (Chuo cha Taifa cha Uongozi) wengi wa waheshimiwa hawa walipata mafunzo yao kati miaka ya 70 hadi 80 mwanzoni.

Walipatiwa mafunzo ya kijeshi pamoja kozi maalumu kwa ajili ya kuwandaa kuwa makada wa siasa, baada ya kumaliza mafunzo yao walipewa cheo cha Luteni usu na kuanza uongozi wao wa siasa za CCM ndani ya Jeshi (JWTZ).

Baada ya Tanzania kuamua kufuata siasa ya vyama vingi wakuu hawa walilazimika kuchagua kubakia Jeshini au kuendelea na siasa, natumaini ni wote waliamua kubakia kwenye siasa na hivyo kuondoka JWTZ. Napenda kukuondoa wasiwasi kuwa hawakujipachika vyeo hivyo.

Natumaini nimekidhi kiu yako
 
Back
Top Bottom