Nina wasiwasi na wataalamu tulionao kwenye wizara ya Elimu kuhusu Elimu zao

Nina wasiwasi na wataalamu tulionao kwenye wizara ya Elimu kuhusu Elimu zao

kabila01

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2009
Posts
4,235
Reaction score
4,964
Nimependa kujitokeza kwa majozi mazito katika ukurasa huu kuwatetea wananch jinsi mambo yalivyo katika wizara ya elimu ambayo ndo tunaitegemea kama dira ya elimu na maendeleo hapa nchini
wao kama ndo viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza wizara ya elimu nina wasiwasi na elimu zao
Ni hivi karibuni wizara imetoa matangazo ambayo imeyatuma kwa wakuu wa vyuo vikuu kote nchini ikiwataka wanafunzi mbalimbali ambao wanasomea fani tofauti na Ualimu watume Maombi wizarani ili wapewe kazi za kufundisha katika mashule mbalimbali hapa nchini. wazo hilo ni zuri
wasiwasi wangu unakuja pale walimu ambao walikua kazini walipoomba kwenda kusoma fani zingine waliambiwa kua watakaporudi hawatatambuliwa kwa elimu hiyo waliyoenda kusomea
 
Sina uhakika kama nimekusoma vizuri concern yako mkuu....!

BWT.....Hii inakuwaje breaking news?
 
Wasiwasi wako ni walimu kutotabuliwa kwa elimu zao nje ya fani ya ualimu au maamuzi ya wizara kutangaza ajira kwa watu sio professionals?
 
..si tu hawataitambua pia utaandamwa na kukejeliwa mpaka ukome!
 
Ni wizara kutangaza ajira kwa watu ambao sio professional na kuwapa stress wale ambao ni professional kiasi kwamba asilimia kubwa wameamua kutafuta kazi sehemu nyingine ambako wanaona watatambulika. sasa hapo wizara inajenga au inabomoa. ilitakiwa kuwawekea mazingira mazuri ili wasiondoke katika fani zao na kuendeelea kubaki na idadi kubwa ya walimu. vinginevyo tatizo la walimu mashuleni kamwe halitaisha kwani hata hao wenye fani zingine wanaenda pale kama kujishikiza wanapotafuta kazi zingine na isitoshe hawana skills za kufundishia
 
Back
Top Bottom