Nina wazo hili, naomba ushauri

juakal

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
587
Reaction score
123
Wakuu nimejichanga nikapata kiasi flani cha pesa. Sasa nataka nitumie hii hela kujenga chumba babu kubwa cha duka na stoo hapa mtaani kwetu.
Itanigharimu kama 5 million maana kiwanja tayari kipo. Na hadi hapo nitakuwa nimeishiwa cash.

Sasa nataka nikishajenga nitumie hilo jengo kama dhamana ya kupatia mkopo, na nifungue biashara hadimu katika eneo hili kama nilivyo survey.

Haya ni mawazo na mipango yangu, nimeona ni vizuri nililete hapa maana wapo wenye uzoefu na taaluma mbali mbali. Kwahiyo naombeni ushauri wenu katika hili.
Pia naomba kufahamishwa taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa mashariti na riba nafuu.

Natanguliza shukrani.
 
5mil utajenga Nyumba ya maana???
Pia sidhani kama benki itakukopesha tu fedha Kwasababu una Nyumba!
Watahitaji uwe na biashara yenye cash flow inayoendana na fedha unayoomba!
Nyumba ni Collatelar just in case biashara imeshindwa kurudisha mkopo basi collateral itapigwa mnada!!!
 

Asante mkuu. Kwahiyo benki haimkopeshi anayeanza biashara?
 

Kwa Maelezo hayo utakuwa umepotea,huwezi kutumia akiba yote kujengea.
ukitegemea mkopo kuanzisha biashara
Nakushauri tumia hiyo 5m kuanzisha biashara baada ya mafanikio,ufikirie kujenga.
 
tumia nusu ya hiyo hela kubuni biashara itakayokuwa inakuingizia kiwango cha uhakika,kama ni mgahawa au bodaboda uipige bima kubwa ili faida ndio ujenge, ile nusu ikae kama akiba au unaweza jenga lakini finishing ukaifanya kwa hela za biashara mwisho utakuwa na nyumba na biashara.
 
Kwa Maelezo hayo utakuwa umepotea,huwezi kutumia akiba yote kujengea.
ukitegemea mkopo kuanzisha biashara
Nakushauri tumia hiyo 5m kuanzisha biashara baada ya mafanikio,ufikirie kujenga.


Asante sana kwa ushauri. Nitaufanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…