Nina wazo la kipekee sana litakaloanza hivi karibuni ila nina hofu kubwa sana

Nina wazo la kipekee sana litakaloanza hivi karibuni ila nina hofu kubwa sana

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Nina aina ya Biashara yangu ndo napambana kuanzisha wakati wowote ila nina wasiwasi sana na hii Biashara na wasiwasi sio kwenye kushindwa au kukosa soko hapana.

Wasiwasi wangu ni kwamba huenda makampuni makubwa yaka copy na kuanza kuzalisha na nikajikuta nafunga biashara.

Nina uhakika kuna makampuni kama Azam, au MO au wakina Jambo food, na wengine wanao zalisha Drinks na Vyakula watacopy mapema sana na hao wana mitaji mikubwa sana.

Ingawa hadi dakika hii hio Idea hakuna sehemu iko implemented nchi hii ila punde nikifungua watu macho nina uhakika nitashindwa kwa sababu wataingia Giant wenye pesa na kila kitu.

Kuna wakati nawaza kuipiga Chini ili nisije wafaidisha hao Giant, na kuna wakati nasema potelea mbali.Make nisha jaribu mara kadhaa kuipiga chini kwa sababu hio ya kuhofia kukopy.

Na Copy ninayo ihofia sio ya watu wadogo hapana nahofia makampuni kama MO au AZAM au wengineo. Hawa ndo ninao wahofia mno

Kwenda kuwauzia Idea siko tiyari kwa sababu Bongo kuuza Idea ni ujinga na unaweza usifaidike chochote na hakuna sheria za kumlinda mtoa Idea.

Hata yule Mkenya Mwanzilishi wa Mpesa nazani leo hii anajuta vibaya mno kwa kuwapa idea Safaricom.

Kwa kifupi Africa ukiuza Idea utakuwa masikini tu.

Nisaidieni.
 
Mbona hata sisi umetuficha unadhani tutacopy idea Yako hapa tuifanyie Kazi kabla yako

Ndo asili ya mtu mweusi lkn
 
Kwa hiyo unadhani unaweza kuwaza kitu ambacho hamna aliyewahi kuwaza? Unless iwe new invention uwe na uhakika kuna watu wengine kadhaa walishawaza.

Kabla ya kuogopa kuibiwa inabidi uogope kuingia sehemu ambayo yawezekana hao unaowaogopa walishafanya utafiti wakagundua hapafai.

Pili kama ni kweli idea ni mpya usiogope mtu mwingine kuifanya. Kuna Coca cola lakini Pepsi yupo na bado kuna Soda za akina Bakhressa, Mo, et al.

Idea moja hata ikifanywa na watu 10, lazima wataifanya tofauti. Kulingana na walivyofanya watakuwa na wateja tofauti. Toka kafanye idea mapema ili kama kufeli ufeli mapema na ujue cha kufanya.... mapema!
 
Unajua hata wakina Mo na barressa bado hawajaweza ku feed soko la tanzania kwa product zao???

Wewe anzisha fikiria miaka 5 mbele

Competition is good for business kama umeweza kubuni wazo ambalo unaliita ni unique na bora hiyo inamaana wewe ni mbunifu sasa mbunifu gani anaogopa competition kwenye nchi ambayo watu wapo busy na umbeya
 
Wewe kama una wazo toa! Acha kuremba mda ndio huu!
 
Idea alone are not protected by law unless there is an expression of words. Find advocate he can assist u bt make sure u pay consultation fee and other fee for registration process.
 
If you can’t compete with them, join them🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
 
Duh..noma sana mzee hongera kama unakuja na ubunifu mpyaaa ambao haupo..Mungu akusimamie maana inaonekana kichwa chako sio cha kawaida
 
Fanya tu baba! Watakopy watauza na wewe utapata kujifunza zaidi na utauza pia!
 
Premature Business Idea - PBI.
TAFADHALI CHUKUA HATUA vyenginevyo utawadha na hatimae kufa na Ideas zako bure bure bila ya jata kuwafaidisha wapendwa na maadui zako
 
Uaitegemee patent yako italindwa
Kama una mtaji anza tu hakuna kitu kinavyumbuliwa siku hizi duniani eti ikawa ya mtu mmoja
Mtu anachukua idea yako anakwenda China anaibadili kidogo na inaingia sokoni
 
Back
Top Bottom