Ninachowakubalia Wakurya ni wananchi wasema ukweli ni wawazi. Hakuna kabila lenye upendo kama Wakurya na wachache tunawaelewa vibaya. Ni wananchi waungwana sana. Ninachokiona kwenye Jimbo la Tarime Vijijini ni vema Mhe. Waitara anze kufunga virago.
Wamemueleza waziwazi mbele yake kuwa uwakilishi wake kwenye Jimbo hilo hajawatendea haki na wakashauri kuwa kama CCM ikitaka kushinda Jimbo hilo walete mtu mwingine na siyo Mhe. Waitara.
Hii salamu tosha kwa Mhe. Waitara na kama ikipendeza anze kuwaaga Wahe. Wenzake.
Kama zinamtosha basi hicho kiinua mgongo chake akitunze vizuri asijidanganye kuingia tena kwenye kinyang'anyiro watamlia hela zake lakini ubunge hatapata.