Wakulima wa vitunguu, mpunga, mahindi na mazao mengine kwa sasa wanazidi kuchanja mbuga kwenye mbio za utajiri. Ndani ya miaka mitatu kilimo kimezalisha mamilionea wengi. Siku hizi ni kawaida ukapita sehemu ukakuta Petrol station au hotel ya kitalii ukaambiwa ni ya mkulima fulani.
Kwa miaka mingi kilimo kimekuwa kikionekana ni kazi ya kimaskini na watu wenye ndoto ndogo. Ilifika sehemu kuitwa mkulima ilikuwa kama tusi. Hata mtu kuitwa MSHAMBA ni matokeo ya kilimo kuonekana kazi ya hovyo.
Kwa sasa wakulima wengi wanachimba maji yao wenyewe na kufanya kilimo bila kutegemea mvua. Kwa mfano wanapolima vitunguu huko Chekereni, Kilimanjaro na Mang'ola, Arusha kwa sasa kuna ongezeko kubwa la mashamba yanayotumia maji ya kuchimba. Zamani watu waliuana kugombea maji ya mfereji.
Kwa dhati kabisa niipongeze serikali ya awamu ya 6 kwa kuwa karibu na wakulima na kuweka miundombinu vizuri. Maeneo mengi ya kilimo kwa sasa yana utulivu hali inayowafanya wakulima kufanya kazi zao kwa ubora wa hali ya juu. Mungu mbariki Mama Samia. Amen