Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 993
Hii ni powertiller, ni kama tractor ndogo ya mkononi, inalima na inaweza kufanya kazi kama planter pia. Unasemaje mkuu?Hivi ni planter? Nifahamishe mdau basi.
Ina thamani ya sh ngapi?
Mtu anayetaka kukukopesha atakuwa na hakika gani kama utaweza kumrudishia pesa zake na hiyo riba?
1. Sijajuwa bei yake ya sasa hasa, lakini ni kati ya mil 2.5 hadi mil 5 inategemea unanuwa wapi.
2. Labda anaweza kunitaka mashahidi na tukafanya makubaliano kwa njia ya maandishi tu.
Karibu mkuu.
Inatia wasiwasi kama kweli umejipanga vya kutosha. Kama hujui ni kiasi gani machine inauzwa unajuaje utaweza kurudisha deni na riba. Ni vyema ungeonyesha mchanganuo wa biashara yako ya kilimo ili watu waweze kukusaidia
Habari Wakuu,
Ninahitaji kampuni au mtu anayeweza kunikopesha mashine hii hapa kwenye picha, nahitaji chombo chenyewe kama kilivyo na siyo pesa lakini sina dhamana. Nitalirejesha deni hili (katika fedha) baada ya miezi 6 na nipo tayari kulipia riba ikiwa itakuwepo
Aliyetayari kunisaidia nitashukuru, nipo dar kwa sasa ila nikiipata tu naelekea mbeya.
Shukrani