Mi najua mtu anahama mwezi wa tatu mwishoni maeneo ya sinza. Nyumba vya kulala ni viwili. Kimoja ni kikubwa ila ndani kuna bafu tu choo inabidi uende nje ila kama fedha zipo utaweka mwenyewe choo ndani mtakatana kwenye kodi ya pili kama utataka. Sebule ipo nzuri tu na jiko pia. Maji ndani hakuna bomba liko hapo nje. Upande mmoja kuna fence ya ukuta kwingine hakuna ni michongoma. Hana gate ila nafasi ya kulaza gari moja ipo na anaekaa sasa hivi gari analaza hapo nje tu hakuna wizi. Hata majirani wengine wanalaza nje ila kuna mmasai analinda. Ukitaka ulindiwe walindiwa ila anaekaa hapo halindiwi na mmasai gari yake inalindwa kwa nguvu za mungu na haijawahi kuibiwa labda kwa vile sio kali kiivyo labda ndo maana anaona hawawezi kukwiba, laki mbili unusu hadi sasa sijui kama itapanda au la maana wenye nyumba nao hawakawii kupandisha