Mie pia napenda kufaham hiyo kitu.Ni wadau gani wanatoa au kupokea hiyo proposal na kutoa hela mkuu
Wadau kama wafanyabiashara , Taasisi na wahisani kutoka nchi za nje,
Unapaswa kuelezea namna gani unahitaji huo ufadhili na umuhimu wake au mahitaji n.k
Mfano kipindi nasoma chuo nilikua waziri wa michezo na chuo chetu kilikua na uhaba wa vifaa vya michezo kama jezi, mipira, bipsi n.k
Hivyo niliandaa proposal nikapeleka Vodacom, NMB, Tigo , wafanyabiashara (sitawataja) so baada ya hapo nilifanikiwa kupata jezi pair 6, vifaa mbalimbali n.k
Mfano , tuseme unataka kujenga kituo cha zahanati katika kijiji fulani kutokana na shida wanazokutanazo wananchi wa eneo husika hivyo wewe eneo unalo na umekidhi vigezo vya wizara kwa mtu anayetaka kuanzisha zahanati
Hivyo utaandaa proposal kuonyesha takwimu idadi ya watu eneo husika, umbali wanaosafiri/kutembea kufuata huduma, idadi ya akina mama wajawazito ambao wamepoteza maisha kwa kukosa huduma za karibu n.k
Kuna watu wanahela lakini hawajui wapi wapeleke so ww andaa proposal peleka,
Cha msingi uwe mwaminifu