Ninaipinga Sheria ya VAR

uncle

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2007
Posts
325
Reaction score
184
Ingekuwa amri yangu hii sheria ya VAR ningeifutilia mbali kwani inalalamikiwa sana na haitendi haki kabisa. Wapi uliona mpira unaamuliwa kwa video refarii? Inapunguza msisimUko wa soka. FIFA wafanye haraka ifutwe kwani ikianza kutumika duniani kote ni janga.
 
Tunakokwenda hiyo VAR itakuwa na VAR yake...halafu matokeo yataamuliwa studio.
 
Kuna mechi spurs v watford
VAR Decision=No goal
On ground Refferee=Goal
Sasa hapo tumwamini nani? Lile goal la Arsenal jana VAR imekataa lakini mimi mtazamo wangu ni goal au ilibidi Arsenal wapewe penalt.
 
Kuna mechi spurs v watford
VAR Decision=No goal
On ground Refferee=Goal
Sasa hapo tumwamini nani? Lile goal la Arsenal jana VAR imekataa lakini mimi mtazamo wangu ni goal au ilibidi Arsenal wapewe penalt.

Kwahiyo mumekua mukipiga kelele pale mambo yanapokwenda vibaya tu? Hivi VAR ishazipa haki timu ngapi ambazo zilikua zishanyongwa tayari? hamulioni hilo?
 
Arsene Wenger aliiona kitambo sana kipindi kile wanaipa promo na haijaanza kutumika

Akaikataa na kutoa sababu zake kuwa itapoteza ladha ya soka ndio kilichopo sasa
 
naona yanga baada ya kusikia var itatumika kwenye mchezo wao ujao na Simba wameshaanza kutoa sababu kutokana na wachezaji wao wahuni kina yondani na jinsi wanavyobebwa wanajua wataumbuka
 
Kuna mechi spurs v watford
VAR Decision=No goal
On ground Refferee=Goal
Sasa hapo tumwamini nani? Lile goal la Arsenal jana VAR imekataa lakini mimi mtazamo wangu ni goal au ilibidi Arsenal wapewe penalt.
Kwani wewe ulikua uwajani live au nawewe ulikua kwenye video kama VAR........utaikubali je kama huo sio ushabiki
 
Kwani wewe ulikua uwajani live au nawewe ulikua kwenye video kama VAR........utaikubali je kama huo sio ushabiki
Sikuwa uwanjani sawa sawa na mtu anayecontrol VAR. Nilichokiona mimi ndicho hicho alikiona yeye, tofauti tu ni kuwa alinichagulia cha kunionesha na pia yeye aliona kwa angle nyingi zaidi.
Kuna muda mimi mtazamaji ambaye nipo tandale kwa tumbo naona makosa kuliko refa ambaye yupo old traford kwa sababu yeye anaona kutokea upande mmoja na pia hawezi kuona offside kwa uhakika.
 
Pamoja na yote kuna sehemu wanakosea control room. Mfano mzuri hiyo mechi ya juzi kati ya Arsenal na Crystal palace
 
Na ikifika Tanzania tunamuweka Mzee wetu Jecha kwenye controls pale
 
Yaani ifutwe kwa hoja ya msisimko?.Duh aisee!
 
iachwe ije hatutaki magoli ya Tambwe ya kufunga kwa mkono au goli la Ajibu lilivyokataliwa Simba na yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…