Nimekuwa nikifuatilia utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndugu Chacha ni mfano wa kuigwa. Anafanya kazi kwa manufaa ya wananchi wote wa Tabora. anaenda kila Wilaya kusikiliza kero za wananchi na kutolea majibu au suluhisho.
Mfano hai ni ufuatiliaji wa magunia ya kuwekea tumbaku yaliyoibiwa. Kwa juhudi zake amefuatilia akiwa na timu ya Ulinzi wa Mkoa na mpaka magunia hayo yakapatikana na baadaye kugawiwa kwenye Vyama vya Msingi.
Funga kazi ni pale alipowaumbua vijana wa TANROADS wanaosumbua wananchi kwenye mizani kwa kuchukua rushwa na kuweka mfukoni.
Kwa kweli huyu Mkuu wa Mkoa apewe maua yake. Ni mtu anayetaka haki kwa kila Mwananchi. Mhe. Rais huyu ni Jeshi lako na anakusaidia sana pale Tabora.
Naomba sana mtie moyo na hata ikiwezekana apandishwe cheo kwa kazi nzuri anayofanya.