Hayandiomaisha
Member
- Oct 1, 2013
- 30
- 10
"Unajua ni hatari sana sisi kuwa wakweli?"
"Kwa kazi zetu hizi lazima tuwe waongo waongo ndio tueleweke unajua..."
"Lakini mbona wa kule magharibi sio waongo waongo? na mbona wakiahidi wanatimiza?"
"Wee wale wananchi wa kule hawaelewi ahadi za uongo"
"Ahaa kwa hiyo tatizo ni wananchi ee."
"Ngoja kwanza,"
"Kwani utaifa kwa hawa wa kwetu ulienda wapi?"
"Aaah hawa wakwetu bwana.. wanaangalia maisha yao ya kijamii tu."
"Utasikia "Mimi sina muda wa kugombana na mtu, ilimradi ninakula vzuri, ninalala,ninavaa vizuri baasi... maisha ndio haya haya."
Aiseee kwa hiyo wafia nchi waliondoka na kinjekitile sio..
"Yaani hawa wa sasa hawana muda kabisa na sijui kama siasa za maji machafu zitaisha kwa namna hii."
Unajua hawa wa kwetu wanasuburi atoKee mtu afanye kitu halafu wampigie makofi. Cha ajabu akikutana na mkono wa chuma wanaanza tena kumsema vibaya.
"Huyu nae amezidi si akae na familia yake atulie!"
"Naona suala la kujitoa sadaka kwa utaifa wao halipo kabisa. Hawa wanalalamika tu halafu ni wepesi sana kusahau."
Hawa wakiumizwa na mfumo wanalia sana lakini machozi yanakauka haraka kisha wanazoea maumivu. "Wanaishi nayo yaani..."😳
'Unajua wale weupe kule magharibi hawawezi kuzoea maumivu. Wao hata kabla hayajawafika shingoni wanalianzisha na kubadili mfumo." Demokrasia safi inajengwa na viongozi au wananchi? Unakumbuka raisi wa kumi na sita wa Marekani, Abraham Lincolin alisemaje kuhusu demokrasia? Serikali ni mali ya wananchi tena wana uwezo wa kuiweka madarakani na kuichomoa . Hii nguvu ipo wapi, magharibi tu au?
Ningekuwa sikupendi nisingehangaika kukuchukia. Ninakupenda ndio maana hata napata hasira juu yako.
Ngoja tuanzie hapa tena.
Nilikua nimekaa najiongelesha mwenyewe na kujijibu mwenyewe.
Nilikua nimeshasikitika vya kutosha. Sasa hivi nikaona hebu ngoja nijaribu kuzungumza. Hata kama ninazungumza na mtu wangu wa ndani. Kwani nikiongea na huyu wa ndani kuna tatizo?. Si ndio yeye hua anafanya maamuzi mara nyingi?.
Wakati mwingine si ndio huyu hua ananiingizaga kwenye majanga?. Si ndio huyu mtu wa ndani mara nyingi ananiponza?. Sasa kama anaweza kufanya maamuzi mabaya yakanigharimu kwanini nisimshawishi leo tufanye maamuzi mazuri yenye tija?. Kwani wewe hujawahi kufanya kitu halafu baadae ukajiuliza "sasa ndio nimefanya nini? Wanaume hii wataelewa zaidi. Hua unamlaumu nani kama sio huyo jamaa yako wa ndani?
Basi sawa, hebu na wewe jaribu kuzungumza na huyo mtu wako wa ndani uone kama hujabadilisha maisha yako mpaka ushangae!.
Watu wengi hasa hawa wa kusini mwa jangwa la sahara au niseme wa nchi za ulomwengu wa tatu, wanaishi maisha ya kutamani. Kila siku wanatamani wamiliki vitu fulani. Kila siku wanaishi kwa kutamani wafike sehemu fulani. Mbaya zaidi wengi wanaishi kwa kutamani kubadilisha hali fulani lakini wanaishia kutamani tu. Wanabaki kutamani lakini hawabadilishi kitu.
Kuna watu wametamani kuandika vitabu, lakini hawajaandika na wameshazeeka. Wengine wametamni kuimba na nyimbo wametunga, lakini hawajaenda hata studio. Leo wanabaki kuwakosoa waimbaji maarufu ambao wameshatoboa na wapo masikioni mwao kila siku.
Kwanini kutamani badala ya kufanya. Wananchi wa bara letu hili lenye pembe kwa pale juu, wana maumivu mengi, maumivu ya kijamii ,kisiasa na kiuchumi. Wakati mwingine hata maumivu ya kiutamaduni. Lakini hawataki kuleta mabadiliko. Wanalalmika tu halafu wanasahau. Inakuwa ndio imeisha hivyo.
Siasa ya maji machafu ipo imetapakaa inanuka mitaani. Watu wanaweza kuamua kubadikisha siasa ikawa safi. Lakini nani amfunge paka kengele?. Maisha ya hawa watu yanazidi kuwa magumu lakini wameyazoea na wanaishi nayo.
Wamekuwa kama mwanamke aliyepewa talaka tatu akarudiwa tena kuolewa halafu akapewa talaka tena. Ina maana hawakujifunza mwanzo? Hivi ndivyo mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ilivyowafanya. Imewaoa, ikawa-acha, ikawachumbia halafu ikawaoa tena. Halafu ikawaacha tena. Daah. Wanaolewa wanaachika kwa miaka mitano, ule mwaka wa mwisho wanachumbiwa tena. Wanakubali wanaolewa tena. Baadae wanaachwa tena miaka inapita hali inarudi vile vile.
Hakuna kitu kibaya kama kujifunza kwa maumivu. Je, hawaoni mbali?, Je, wanapuuza, au wameridhika? Sasa wanaridhikaje na maumivu, hali mbaya, masikitiko na wasi wasi?. Hii ni ajabu sana.
Unajua watu wanaopenda uhuru wa kiuchumi na kisiasa, kwa mfano tu. Wakitaka kuwa huru, watakuwa huru tu. Tatizo watu hawa ni wabinafsi. Wanafikiria maisha yao ya sasa tu. Ndio maana nikasema hapo juu, watu majasiri wa kufanya maamuzi bila kuangalia yatamgharimu kiasi gani,waliondoka wakati wa vita ya mjerumani.
Ninachojua mimi, viongozi wengi wa bara hili hawana wasi wasi hata wakifanya ujinga. Wanajua watu wao ni watu wa mihemko, wabinafsi halafu wenye njaa. Hivi unajua ilivyo rahisi kucheza na akili ya mtu mbinafsi halafu mwenye njaa. Kazi ndogo sana hiyo. Hicho ndicho kinawafanya hawa ndugu viongozi kufanya vitu vya hovyo wakijua kabisa hamna mtu wa kuwafanya chochote.
SASA TUNAFANYAJE?
Martin Luther King aliwahi kusema, kuna watu watachomwa moto kwa sababu walinyamaza wakati uovu ukitendeka. Kuna watu wanaweza kuona tatizo na wakalinyamazia kwa sababu haliwagharimu moja kwa moja.
Lakini sasa ukweli ni kwamba....kama binadamu wangeamua kukataa hali fulani kiukweli kweli bila maigizo na kuangalia maslahi, hii dunia ingekuwa mahali salama sana. Jambo hili halianzi kwa mtu mwingine, linaanzia kwako na kwangu. Wanasiasa wanadanganya danganya watu na watu hawana habari. Wangekuwa hawapendi kudanganywa unadhani wanasiasa wanagewadanganya?
Wameamua kupotezea na kupotezea kwao kumewafanya wale wanaowaonea kuendelea kuwaonea bila kufikiria kuacha kuwaonea.
Amka anza kubadilisha mtazamo wako, badilisha watu wa nyumbani kwako, wa mtaani kwako watafuata na mwisho wa siku watu wa taifa lako watabadilika. Mabadiliko ya fikra yanaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa, ya kiuchumi na kijamii. Kama fikra za watu zinaona maisha magumu ni fresh tu, itakuwa ngumu sana kuwashawishi kupigania uhuru wa uchumi wao. Vivyo hivyo katika siasa na masuala ya kijamii kwa ujumla.
Kama andiko hili litaweza kubadilisha kitu kwenye maisha yako nitafurahi sana kwani hilo haswa ndio tamanio langu. Mungu akubariki sana na ninakutakia utekelezaji mwema. Asante"Kwa kazi zetu hizi lazima tuwe waongo waongo ndio tueleweke unajua..."

Upvote
0