Kitu ambacho kinanifanya nimpende Diamond ni jinsi anavyompenda,mjali na kumuheshimu mama yake.
Mimi kama mwanamke natamani siku nikiwa mama mwanangu anithamini kama ambavyo Dimond anamdhamini mama yake.Nilipenda jinsi anavyokwenda kuchukua baraka kwa mama yake kabla ya kwenda kwenye show zake.
Honestly mimi siamini kama Diamond ni mshirikina,kinachompandisha Diamond ni baraka za mama yake.Kama diamond angekua anafanya vitu vya kumsononesha mama yake na yeye angevuma kidogo tu nakuporomoka kama wenzio.
Pia ukweli Diamond ana sauti nzuri na ni mbunifu.
Kitu anachoniudhi Diamond ni vile alivyoonesha ule mboxer mweupe mbali ya hapo tukimsuport anaweza kufika mbali sana ktk ramani ya muziki wa kimataifa.
Kati ya nyimbo zake ninazozipenda ni Nitarejea.Mashairi ya ule wimbo ni mazito ukiyatafakari kwa undani yanatuhusu sana watanzania.