Sweety Juma
Member
- Nov 8, 2013
- 13
- 10
Salam wana JF. Mimi ni mwanamke mwenye umri miaka 48 ambaye naishi na VVU natafuta mwanaume wa kuishi nae au kufunga ndoa, kama yupo tayari. Awe na umri kuanzia miaka 50-55, kwa ufupi nilikuwa na mume ambae nilimuamini na kumpenda sana yeye ni mfanyabiashara nje na ndani ya nchi baada ya miaka 4 alianza mabadiliko ya kutowasiliana tena na mimi. Mwaka uliofuta nilipata mchumba na tulihitaji kufunga ndoa nikaona niende ANGAZA kuangalia afya yangu lakini haikuwa siku nzuri kwangu kwani nilijikuta nimeshapata maambukizo sikuwa na jinsi. Nilimuomba Mungu katika sala zangu anisaidie na kunitia nguvu katika maisha yangu ya upweke. Kwa vile nimezoea kuwa na mwenzangu kuishi peke yangu ni vigumu kwangu, nami naomba kujitokeza mimi nipo katika ukweli (serious) na tutalindana.