Ninaomba kazi au mawazo ya namna ninavyoweza kupata kazi ya kufanya kwa nusu siku (part time job) hapa Dar

Ninaomba kazi au mawazo ya namna ninavyoweza kupata kazi ya kufanya kwa nusu siku (part time job) hapa Dar

Funny boe

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2023
Posts
1,319
Reaction score
2,334
Habari za usiku huu wanabodi wenzangu na pole pia kwa mihangaiko ya shughuli zenu za kila siku

Kama kichwa cha uzi kinavyosema hapo juu kuwa nilikuwa nawaomba members wenzangu wa hili jukwaa kubwa la JamiiForums muweze kunipatia msaada wa kazi kwa yeyote mwenye uwezo wa kunisaidia au mawazo yoyote ya namna ninavyoweza kupata kazi ambayo nitakuwa nikiifanya kuanzia asubuhi hadi saa 9 alasiri.

Ninaomba kazi au ushauri wa kupata kazi ya kufanya muda tajwa hapo juu (yaani kuanzia asubuhi hadi saa 9 alasiri) kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa chuo ambapo masomo yangu huanzia saa 10 kamili jioni hadi saa mbili usiku, hivyo kutokana na sababu hiyo siwezi kufanya kazi siku nzima.

Ninafanya hivi kwa sababu nahitaji kuwa na uwezo wa kukidhi mahitqji yangu ya kawaida na madogo madogo maana hali yangu kiuchumi kwa sasa sio nzuri

Wasifu wangu; nipo mwaka wa kwanza nikichukua Certificate of Computer Science ndani ya moja ya vyuo humu Dar hivyo maswala ya boom na mikopo kwa wanachuo sikuwa na vigezo vya kupata.

Kijana wa kiume na Nina umri wa miaka 20 tu na ninaweza kufanya kazi yoyote halali ndani ya muda huo kikubwa iweze kunipatia chochote kitu na isiingilie ratiba zangu za darasani.

Ahsante sana na karibuni kwa mawazo yenu yoyote na nipo tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi kadiri ya uwezo wangu.
 
Karibuni sana kwa mawazo na michango yenu.
 
Back
Top Bottom