Ego is the Enemy
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 8,201
- 16,246
Habari wanajamvi!
Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa letu pendwa katika kufikia ndoto ya Tanzania ya uchumi wa kati.
Ninaomba kufahamishwa kuhusu hizo Ishu za gari za mkataba.
Mfano kuna mtu nimeongea naye anadai nimpatie ama nimnunulie Noah nisajili kwa biashara, nikatie bima kubwa aka comprehensive.
Awe ananiletea 50k kwa siku kwa muda wa miaka miwili gari linakuwa lake.
Matengenezo ni juu yake. Hii akili imekuja wakati nikishauriwa kuhusu uzi wangu wa gari.
Mkataba utakavyokuwa:
Mdhamini ni wazazi wake wawili wanaweka hati ya nyumba yao kwangu. huku wakiwa wameapa kwa kiapo kuwa tunaweka hati hii kumdhamini kijana wetu kupewa gari kama dhamana ya mwenye mali likitokea la kutokea nyumbani hii itamlipa mwenye mali pesa yake itakayokuwa imesalia.
Hati nakaa nayo mikononi ambapo naweza nikaamua nikaitunza hata benki kwenye safe zao kwa usalama zaidi.
Maana kuna mtu anaweza akajiteka ama akajiibia baadaye akaja kwako kuelezea kuwa kaibiwa.
Matengezo ni juu yake, mimi miaka miwili ikiisha nampatia hatimiliki na kadi ya gari inabadilishwa inakuwa na jina lake.
Maana nyumba inabidi baba na mama yake wote waape mana hati Iko kwa jina la baba na mama naye ana maslahi na nyumba ivyo ni mazima naye aape kiapo ili asije kulalamika huko mbeleni.
Ninaombeni wenye ujuvi wa mambo hizi mnipe mawazo pia namna ya mktaba unavyotakiwa uwe ili niwe risk free.
Nitashukuru kwa mawazo yenu wana JamiiForums wenzangu. Ninaamini huku hakuna kinachoshindikana.