Ninaomba kufahamishwa kuhusu gari la mkataba

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
8,201
Reaction score
16,246
Habari wanajamvi!

Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa letu pendwa katika kufikia ndoto ya Tanzania ya uchumi wa kati.

Ninaomba kufahamishwa kuhusu hizo Ishu za gari za mkataba.

Mfano kuna mtu nimeongea naye anadai nimpatie ama nimnunulie Noah nisajili kwa biashara, nikatie bima kubwa aka comprehensive.

Awe ananiletea 50k kwa siku kwa muda wa miaka miwili gari linakuwa lake.

Matengenezo ni juu yake. Hii akili imekuja wakati nikishauriwa kuhusu uzi wangu wa gari.

Mkataba utakavyokuwa:

Mdhamini ni wazazi wake wawili wanaweka hati ya nyumba yao kwangu. huku wakiwa wameapa kwa kiapo kuwa tunaweka hati hii kumdhamini kijana wetu kupewa gari kama dhamana ya mwenye mali likitokea la kutokea nyumbani hii itamlipa mwenye mali pesa yake itakayokuwa imesalia.

Hati nakaa nayo mikononi ambapo naweza nikaamua nikaitunza hata benki kwenye safe zao kwa usalama zaidi.

Maana kuna mtu anaweza akajiteka ama akajiibia baadaye akaja kwako kuelezea kuwa kaibiwa.

Matengezo ni juu yake, mimi miaka miwili ikiisha nampatia hatimiliki na kadi ya gari inabadilishwa inakuwa na jina lake.

Maana nyumba inabidi baba na mama yake wote waape mana hati Iko kwa jina la baba na mama naye ana maslahi na nyumba ivyo ni mazima naye aape kiapo ili asije kulalamika huko mbeleni.

Ninaombeni wenye ujuvi wa mambo hizi mnipe mawazo pia namna ya mktaba unavyotakiwa uwe ili niwe risk free.

Nitashukuru kwa mawazo yenu wana JamiiForums wenzangu. Ninaamini huku hakuna kinachoshindikana.
 
Sina gari ila hiyo kwa bei ya 50000 kila siku sawa na hesabu ya hiace hiyo...ni ngumu na kama itawezekana basi hiyo gari itakuwa boksi baada ya miezi 6 maana atafosi sana mwishowe itakosa na matunzo maana kila kitu juu yake.

50000 × 30 = 1,500,00/=

1,500,000 x 24(miezi) = 36,000,000/=

Sina gari ila fikiria upya mkuu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Macho yangu yamekwenda moja kwa moja kwenye hyo miekundu mitano.
(50,000 × 730) - Gharama za ununuzi wa gari & bima = FAIDA
 
feyzal,
Kwa lugha nyingine jamaa amekopa milion 14 au 15 bei ya Noah japo hatujui model na anapaswa kulipa milioni 36,500,000/= ndani ya miaka 2
wataalam hapo interest ni ngapi?
 
Nimeshafanya hii biashara,
Wanakuwaga na mawazo na mipango mizuri sana wakati wanakuja kwako na pendekezo la aina hiyo.
Tatizo utaliona pale mtakapoanza huo mkataba ndipo hadithi zitakuwa nyingi kuliko pesa.
Tuwe realistic, hakuna namna Noah inaweza kuleta hesabu ya elfu 50 kwa siku kila siku,
Mnachoweza kufanya hapo ni kukubaliana kila mwezi akulipe kiasi gani kisha kugawa kiasi hicho kwa wiki au siku, kisiwe kikubwa sana na aweze kulipa kidogo kidogo.
Usidanganyike na utayari wa wazazi kumdhamini kwa nyumba, unaweza kujikuta unajiingiza kwenye matatizo zaidi.
 
Ngoja tuwasubiri ila hiyo gari lazima ipondwe hasa elfu 50 kwa Noah sio mchezo halafu hapo hapo matengenezo na matunzo juu ya dereva
feyzal,
Kwa lugha nyingine jamaa amekopa milion 14 au 15 bei ya Noah japo hatujui model na anapaswa kulipa milioni 36,500,000/= ndani ya miaka 2
wataalam hapo interest ni ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar mleta mada. Nafikiria kwanza angalia bei ya noah hiyo,jumlisha bima kubwa na faida unayoitaka kwa mwaka mmoja then gawanya kwa miez 12 ndio yawemalengo ya huyo jamaa. Vile vile hela alete kwa wiki sio kwa siku coz kuna siku hata pata sana hela na kuna siku atapiga hela.
Pia angalia mazingira ya huko kwenu je Noah inaleta hela? Je hakuna gar nyingine kama carry inaweza kupiga kazi na mkapata hela? Je wewe mwenyewe hauwezi kufanya hiyo kazi yaa kuendesha hiyo gari badala ya kumpa mtu kwa mkataba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewaza Kama mimi aisee.
Mwisho wa siku watagombana tu na pesa zake mwenyewe zitaanza kumtesa kuanza kupelekana polisi kila mara.
Kama hesabu ya 20k tu ya taxi ni pasua kichwa hiyo 50k ataipata kwa njia gani?Hili ndio Jambo la kwanza la kujiuliza kabla ya mambo yote.
Ingekuwa rahisi hivyo kila mtu angehamia kwenye hiyo biashara apate hiyo milioni 36 kwa miaka 2.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ndicho ninachokiona.
Muda mwingine wazee huwa wanasaini tu kwa kumfurahisha mtoto wao bila kujua effect ya mbeleni.
Baadae sheria itakapochukua mkondo wake hao ndio watakuwa wa kwanza kuandamana kwenda kwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa na kutangaza unyanyasaji kwa kuchukuliwa sehemu yao wanayoitegemea kulala.
Ni vema Kama ana pesa iko idle afikirie biashara nyingine ya kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu Ndugu yangu bora ununue Hiace ila kwa Noah utaitesa ndugu utaishi kwa stress...

Ila haya labda utakua una uzoefu wana Jf wanakutakia mafanikio ndugu muhimu usisahau kutupa mrejesho ili watu wajifunze kwako
Anaiweka kwenye ruti ya Karatu to ARUSHA. Ndo hesabu zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo dereva mbona mjinga hivyo. Hela nyingi sana hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…