Mtoa mada aliulizia anaye mfaham Mayanga! Huyu jamaa amechezea Mtibwa tangu ikiwa daraja la tatu hadi ilipopanda daraja la kwanza miaka ya tisini! Na alikuwa nahodha wa mtibwa tangu timu ikiwa daraja la tatu mpaka alipostaafu soka miaka ya mwanzoni mwa 2000 alipomwachia unahodha Meck Mexime! Wakati timu ikiwa daraja la 3 alicheza kama kiungo mkabaji lakini baadae alicheza zaidi kama beki wa kati! Jamaa alikuwa anacheza sana mpira wa kibabe!
Salum Shabani Mayanga mzaliwa wa Morogoro mjini ndiye alikuwa nahodha wa Mtibwa wakati ikichukuwa ubingwa wa bara ' back to back' mwaka 1999/2000! Anaelimu ya kutosha ya ukocha kwani alipata mafunzo ndani ya Tanzania na nje ya nchi katika nchi kama Brazil na Ujerumani! Mwanzoni alikuwa kocha wa kikosi cha Pili cha Mtibwa na kisha kocha msaidizi na baadae akawa kocha mkuu!
Baada ya Meck kustaafu alikuwa msaidizi wa Mayanga lakin walishindwa kufanya kazi pamoja kutokana na Meck kujiona anajua kuliko bosi wake! Ikabidi Mayanga aondoke na Meck akawa kocha mkuu! Mbali ya Mtibwa Mayanga aliwahi kufundisha Kagera sugar na Tanzania Prisons ya Mbeya! Na pia ndiye alikuwa kocha wa ile timu iliyoitwa taifa stars maboresho! Licha ya kwamba Mayanga amecheza na kusomea mpira ktk kiwango cha juu bado sio kocha mzuri hata kwa kumlinganisha na Meck Mexime! Ni bora atimuliwe arudi Mtibwa ambako mpaka sasa bado ni mwajiriwa wa kiwanda hicho kama Afisa ustawi wa jamii! Kimsingi Mayanga ni mtu wa mpira haswaa sijui tatizo liko wapi?
Sent using
Jamii Forums mobile app