Kumekuwa na wimbi kubwa la ufugaji wa samaki Kanda ya Ziwa na hasa Jiji la Mwanza. Masoko mengi jijini Mwanza yamejaa hawa samaki wanaofugwa na ndiyo wanauzika kwa wingi.
Ninaomba kuelemishwa kama hawa samaki ni salama kwa kuliwa kwa ajili ya afya zetu. Wachina ndo wamejenga viwanda vya kutengeneza vyakula vyao. Samaki hawa wasije wakafanana na kuku wa kisasa ambao kwa asilimia kubwa siyo salama kwa afya ya binadamu kutokana na chakula wanachopewa. Ninaomba Watalaam wa afya watuhakikishie ubora wa samaki hawa.