BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,122
- 4,060
Salamu waungwa Wana Sheria. Ninaomba msaada wenu ili niweze kumsaidia Baba yangu mdogo tatizo lake linalomsumbua.
Kwa miaka 28 hadi anastaafu baba yangu mdogo ametumia jina lake, na ili tatizo lake lieleweke Vizuri ninaomba kutumia jina la mfano kwamba alikuwa anatumia jina LA JOHN SMITH.
Tokea akiwa kazini baba yangu mdogo akawa na biashara zake za hapa na pale za kujiongezea kipato ambazo ili kuepuka mgongano na Mwajiri wake akawa anajiita ROBERT SMITH.
Baada ya kustaafu akawa anatumia rasmi jina hilo akijua ameishamalizana na ajira anangoja pensheni take tu.
Hata yalipokuja mambo ya vitambulisho vya Kura na NIDA ahawa amejiandikisha kwa jina lake ambalo jamii inamfahamu nalo zaidi la ROBERT SMITH na sio lile alilosomea na kuajiriwa la JOHN SMITH jamii inayomtambua nalo.
Shughuli imeanza kwenye Mafao ambayo sasa kila mwaka wanatakiwa kwenda Taasisi ya Akiba waliyomo ili Kuhahakiwa ili waendelee kupata pensheni yao.
Shughuli inakuja hapo:
Je, Baba mdogo anaweza kutoa no ya NIDA ya ROBERT SMITH aliyonayo ili kuhakikiwa kuwa ni JOHN SMITH muajiriwa anayestahili kupata mafao yake?
Kwa vile sasa umekuwa ni fasheni ya kila Taasisi ya Huduma kutaka vitambulisho ama no ya NIDA, ikiwemo Benki anakopitishia pensheni yake, je anatakiwa kufanya nini?
Je atakapotumia no ya NIDA aliyo nayo kwa jina la ROBERT SMITH ili kumhakiki JOHN SMITH, itamletea matatizo gani, potelea mbali kwamba Ni mtu mmoja huyo huyo?
Je kwa case kama hii baba mdogo anapaswa kufanya nini ili aendelee kupata pensheni yake??
Baba mdogo anatakiwa kwenda kuhakikiwa mwezi ujao March kama yeye ndiye JOHN SMITH kweli. Mikataba ya ajira yote IPO kwa Nina lake alilosomea na kuajiriwa lakini no ya vitambulisho cha NIDA ipo kwa jina la ROBERT SMITH, Nina analotumia kwenye Biashara zake.
Je anafanyaje hapo? Ninaomba Msaada wenu waungwana Wana Sheria...maana Baba Mdogo ameishaanza kupata Stress kutokana na hili.
Nidokeze tu hapa kwamba ana Miaka 65.
Nawaombeni Msaada wa Ushauri.