Ninaomba msaada kwa gharama yeyote Nawasihi

Ninaomba msaada kwa gharama yeyote Nawasihi

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
10,805
Reaction score
14,181
Mhali gani ndugu,mimi baba yangu anaumwa kisukari aina ya Type 1 ,niko tayari kwenda kokote duniani nimpe zawadi ya kupona ameshatumia insulin kwa miaka minne sasa kwenye mitandao nimezunguka sjapata mwanga ,naomba mungu awaongoze mnitolehi hili hangaiko kuu
 
Toa mashaka kabisa,kisukari kuna watu wanapona kabisa walio jaribu kutumia product za forever living,wana product mbalmbal kama naturemin hii ni product ambayo ina chromium inayo isaidia insulin ifanye kazi yake effectiv to utilize glucose na kupunguza tatizo la diabetes,ni pm number yako tujaribu ona kama we can help your beloved daddy,nipo dar,sijuwi wewe upo pande zipi?
 
Chunga sana matapeli.Kisukari hakina dawa mimi ninacho fwata ushauri wa madaktari tu.Nina pesa za kutosha ila hakuna dawa.
 
Dawa pekee ya sukari ni kufuata ushauri wa daktari ambao ni
Dawa; diet; na therapy kwa ajili ya kumsaidia kukabiliana na sonona (depression) kucope na sukari pamoja na msongo wa mawazo ndicho kitakachomsaidia baba yako
Ogopa wanakudanganya kuna tiba! Ni waongo!
Msaidie kufuta ushauri wa dr. Hapo utamfanya aishi maisha marefu
 
Hakuna tiba wala dawa ya kisukari baba yangu kaugua kisukari mwaka 2000 kafariki mwaka huu tumehangaika nae sana bila mafanikio, kwa Ushauri wa haraka kuna Dr. Anaitwa ABBAS yupo k/koo karibu na fire ana clinic yake pale inaitwa abbas medical centre special kwa wagonjwa wa kisukari tuuu huyu muhindi ni mwisho wa matatizo....
 
pole sana,,,but hakuna tiba za kisukari ile kinachotakiwa hiyo sindano ya insullin asiache kutumia then its better zaid akiwa anapima mara kwa mara blood sugar iko kias gan before using insulin coz kuna sku zingne sukar huwa inakuwa normal,,then ajitahid sana kutokula vitu vya sukar nying ,afanye mazoez mara kwa mara,,,asante na apunguze stress about diabetic mellitus aendelea na kaz zake za kawaida za kila sku,,hapo ataishi kama kawaida.
 
Pole Sana ndugu yangu.mzee atapata nafuu
 
Kisukari Hakitibiki. Japo Watu Wanaweza Kubadilishwa Kongosho Ambao Ni Upasuaji Wenye Risk. Cha Muhimu We Hakikisha Anapatata Huduma Bora Kabisa Mfano Mnunulie Insulin Pump, Hakikisha Madaktari Anaowaona Ni Wale Mabingwa, Hakikisha Ana Vifaa Vya Kupinmia Blood Glucose Mara Kwa Mara, Hakikisha Anaonana Na Wataalamu Wa Macho Na Moyo Mara Kwa Mara.Na Wewe Hakikisha Unajitahidi Kuelewa Kisukari Kadri Uwezavyo.
 
nasikia mijohoro ikichanganywa na baazi ya miti inatibu kisukari embu jaribu. inapatikana kwenye maduka ya dawa za asili
 
Poleni sana kwa kumuuguza Mzee wetu, najua kiasi gani unapigania afya ya Baba iwe sawa ila Uwe makini sana hasa Mataperi hasa wanaposikia uko tayari popote Duniani kwenda ili umzawadie Afya njema Baba.
 
Jamani kuna tiba ya kisukari. Niko tayari kutoa pesa nimnunulie mtu product atumie ikimsaidia anirudishie! Nasema hivi kwa sababu nina shuhuda nyingi za watu waliopata msaada. Wasiliana nami kwa 0716 299 399.
 
Back
Top Bottom