Wana jukwaa! Nilinunua laptop mwaka 2008 ikiwa inatumia windows vista basic. Miezi michache iliyopita niliipeleka kwa mtaalamu mmoja akanishauri nibadilishe windows na akaniwekea windows 7. Cha ajabu ni kuwa baada ya kuwa natumia internet mara kwa mara kuna mabadiliko yametokea. Kwanza screen imebadili rangi na kuwa nyeusi lakini pia kuna maandishi yafuatayo yanajitokeza. THIS COPY OF WINDOWS IS NOT GENUINE. Nifanyaje kutibu tatizo hili, maana hata raha ya kuitumia laptop yangu imeisha. Na jamaa aliyenibadilishia hito windows, kila nikimtafuta ananikimbia.