ISLETS
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 8,120
- 5,352
Naimani weekend imeanza vyema kwenu.
Najua Jf hakushindikani kitu, wapo watu wanaofahamu mambo tofauti fofauti na wanaweza kuwa msaada kwa wengine.
Mwanzo niliipongeza sana serikali(kimoyomoyo) kwa kuleta hivi vitambulisho vya wajasiriamali wadogo nikaona itawaondolea kero na adha ya kodi TRA.
Sasa naona ni kama hivi vitambulisho si kwa ajili ya wajasiriamali pekee bali ni kila raia wa Tz na ndio hapa naanza kuwaelewa GT's wa Jf waliovifananisha na kodi ya kichwa ya enzi za Nyerere.
Mimi ni mfanyakazi wa sekta binafsi, na sina biashara nyingine yoyote kwa sasa, si mjasiriamali. Lakini nimeshangaa kuona watu wa Halmashauri ya mji wamekomaa kwelikweli kututaka na sisi waajiriwa kuwa na vitambulisho wa ujasiriamali, na hapo hapo kuna baadhi ya waajiriwa wao wanavyo hivyo vitambulisho maana wana biashara zao nyingine, ila wanalazimishwa kununua kitambulisho kingine tena kwa kwa madai ya kuwa wanafanya kazi sekta binafsi na hawakatwi kodi mishahara yao.
Hii waungwana wa Jf, wajuzi wa mambo ndivyo hali ilivyo?
Imekuwaje tunaanza kulazimishana kununua vitambulisho wakati sisi sio wajasiriamali?
Je, nchi nzima hali iko hivi au ni baadhi ya maeneo pekee?
Nimeongea na mtumishi mmoja wa umma, naye kasema nao wameambiwa hivyo hivyo kuwa ni lazima wanunue hivi vitambulisho.
Sasa kama hali ndio hii, kwa nini serikali isitangaze tu moja kuea ni lazima kila mtu kununua ili tuelewe kuliko kutumia jina la ujasiriamali?
Kwangu hii imekuwa kero sana, 20000 kwa mwaka si kitu, ila inaboa kulazimishana kwa kusingizia ujasiriamali mara kodi yani hawana maelezo yaliyonyooka.
Privately nikamuuliza mfanyakazi mmoja wa halmashauri, kwamba kwa nini imekuwa hivi, naye analia kuwa nao wanabanwa kwamba lazima watu wanunue vitambulisho, this means kwamba kuna pressure kubwa kwenye hii biashara ya serikali ya vitambulisho na kama utapeli hivi.
Hapa ndio kikakumbuka kuwa, hata RC Hapi hakukutupuka kuwaambia waandishi wa habari kununua hivi vitambulisho. Japo serikali (waziri) alimkana lakini ukweli uko pale pale kuwa alichosema Hapi ndio kilichopangwa na serikali, ila walitaka tu kujisafisha baada ya kumtumia Hapi kama chambo na kuona reaction ya waandishi wa habari ilivyokuwa.
Humi Jf kuna watu wa kila idara ya serikali mpaka Ikulu, hebu fikisheni hizi kero, tupatiwe majibu. Sio waziri akisimama bungeni anasema hili wakati tunachofanyiea wananchi ni tofauti.
NB: Tahadhari kwa watu wa halmashauri wanaokuja kwa biti kutulazimisha kununua vitambulisho, siku mkifukuzwa na mateke msishangae. Hofu zenu za kutumbuliwa zisitukoseshe amani tusiohusika.
Maendeleo hayana Chama.