Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Kama kichwa cha Posti kinavyojieleza, ninaishi Dar es Salaam jiji la joto jingi baridi nadra labda tu ikitokea malaika wa baridi amefurahi kama ilivyotokea mwaka mmoja kati ya 90 ambapo watu waliota moto usiku, hiyo ndiyo hali ya hewa nilipo.
Ardhi ni mchanga zaidi usiojulikana mchanganyiko wake kutokana na tabia zetu mbovu za uchafuzi wa mazingira, hali ya hewa ni moshi mwingi kutokana na magari mengi yanayozurula kutwa kucha kuwa ni mitumba, pia uchomaji wa taka mitaani usioisha, natumai kwa utangulizi huu mtaalamu atanishauri nitumie nini kutatua tatizo la miti yangu.
Hii miti ukifika msimu wa kutoa maua hutoka ila hupukutika katika muda mfupi licha ya kujaribu kupulizia dawa ambayo huenda si sahihi, ombi langu kwa wenye uzoefu na utaalamu mnishauri nini cha kufanya ili kuzuia hayo maua yasipukutike kwani yakipukutika ni mpaka mwaka mwingine ndipo yachanue tena, kumbuka nami nitakua nimepunguza mwaka mmoja wa kula hayo matunda kwani nami ninakua.
Karibuni wataalamu wa miti ya matunda hasa miparachichi.